KAMPUNI ya simu za mkononi  ya TECNO, imezindua  rasmi simu yake mpya CAMON 15 ambayo imesheheni sifa mbalimbali ikiwemo  kamera ya nyuma yenye MP64 na mbele MP32 ambayo imewekewa  teknolojia  kubwa yenye uwezo wa kupiga picha mahali popote na wakati wowote.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa simu hiyo wiki hii jijini Dar es Salaam kupitia mitandao ya kijamii meneja uhusiano wa kampuni hiyo, Eric Mkomoya, alisema  simu hiyo itawasaidia sana watu wanaopenda  kutumia kamera katika nyanja mbalimbali za maisha wakiwemo wafanyabiashara, wanamitindo, wanaopenda utalii wa kusafiri, wafanyabiashara za mitandaoni, waandishi wa habari pamoja na makundi mengine ya kijamii.

“Simu hii TECNO CAMON 15 ina sifa nyingi sana kubwa na zinazoweza kumridhisha mtumiaji, kamera yake ya nyuma ina MP64 na mbele ni MP32 lakini inatunza sana chaji. Kamera ya simu hii ina uwezo wa kupiga picha mahali popote na wakati wowote hata usiku” Alisema Mkomoya.

Meneja uhusiano wa kampuni ya TECNO Bwana Eric Mkomoya
Aliongeza kuwa TECNO CAMON 15 ni tofauti na simu nyingine kwani hii inapiga picha kwa kuchukua eneo pana zaidi kutokana na kioo chake kikubwa hivyo hata kama mtu anapiga selfie ya zaidi ya mtu mmoja hahitaji kusogeleana kwa karibu hasa kipindi hiki cha janga la maambukizi ya virusi vya corona.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...