Jeshi la Polisi Mkoani
Mbeya linafanya msako mkali kumtafuta HAKIMU JAMES MWAKIFUNA miaka [20]
Mnyakusa wa Kiwira kwa kosa la Mauaji ya makusudi ya bibi JUNE
SANKANYE miaka [65] wa kijiji cha Nkunga Kata ya Nkunga {T} Ukukwe.
Tukio hili lilitokea
tarehe 23/04/2020 saa 05:00 Wilaya ya Rungwe. Marehemu ambaye ni bibi mzaa baba wa
mtuhumiwa walilala nyumba moja. Huku
mtuhumiwa akiwa sebuleni na marehemu amelala chumbani.
Usiku muda usiojulikana HAKIMU JAMES
MWAKIFUNA alichukua kitu chenye ncha kali na kumkata bibi shingo na
kumtenganisha kichwa na kiwiliwili na kisha kuondoka na kichwa cha JUNE
SANKANE.
Mnamo tarehe 18/04/2020
mtuhumiwa HAKIMU J. MWAKIFUNA alianza kuvua nguo na kutembea na Panga
huku akitaka kuua baadhi ya ndugu zake aliokuwa akiishi nao Kiwira kwa bibi
mzaa mamaye – MONICA BUKUKU.
Kufuatia hali hiyo tarehe 21/04/2020 alifukuzwa na kwenda kwa
marehemu ambaye ni bibi yake mzaa baba yake.
Baada ya kufanya tukio
hilo mtuhumiwa alitoboa ukuta wa nyumba ya marehemu na kuondoka na kichwa
kwenda kusikojulikana.
Jeshi la Polisi linatoa
rai ni tukio baya sana kutokea mkoani kwetu na kuwasihi wananchi na viongozi
wote wa wananchi popote akionekana mtu mwenye dalili za upungufu wa akili
apelekwe hospitali kupata matibabu.
Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...