Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Dodoma (TAKUKURU) Sosthenes Kibwengo akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake leo kuhusiana na tathimini ya robo ya mwaka kwa mwezi Januari hadi Machi.

Charles James, Michuzi TV
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Dodoma katika kufuatilia miradi ya maendeleo imewezesha mradi wa maji wa kijiji cha Mlongia wilayani Chemba kutoa maji na kuwafaidisha wananchi zaidi ya 5000 ambao awali hawakua na huduma ya maji.


Mradi huo wenye thamani ya Sh Milioni 579 ulianza mwaka 2013 na kukamilika mwaka 2014 lakini haukua unatoa maji hadi TAKUKURU walipofuatilia na mkandarasi kurudi katika eneo lake la mradi na kufanyia marekebisho na sasa maji yanatoka.


Ufuatiliaji huo wa TAKUKURU ulibaini pamoja na mradi kuwa chini ya kiwango pia mkandarasi alilipwa Sh Milioni 120.2 zaidi ya thamani ya kazi zilizofanyika hivyo pamoja na mradi kukamilika pia ameshaanza kurejesha serikalini fedha alizozidishiwa.


Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma leo, Mkuu wa TAKUKURU wa Mkoa, Sosthenes Kibwengo amesema ndani ya kipindi cha robo ya mwaka huu pia wameokoa jumla ya Sh Milioni 297.1 pamoja na kushikilia magari matatu kutokana na ufuatiliaji wa kazi mbalimbali ili kuhakikisha fedha na mali za umma zinatumika kulingana na utaratibu sahihi.


" Sh Milioni 143.5 ziliokolewa kutoka kwa viongozi na wananchama 67 wa vyama sita vya akina na mikopo (Saccos) waliokua wanadaiwa kwa muda mrefu na magari hayo matatu yalichukuliwa kutoka kwa viongozi wa saccos moja waliokua wanayatumia kwa faida binafsi.


Kiasi kilichobaki Sh Milioni 153 kimeokolewa kwa kufuatilia na kurejesha mapato ya serikali yaliyokusanywa kwa njia za kielektroniki lakini hayakuwasilishwa sehemu husika ikiwa ni pamoja na fedha za vitambulisho vya wajasiriamali, mishahara hewa na matumizi yaliyofanyika kinyume na maelekezo lakini pia fedha zilizochepushwa kutoka miradi ya maendeleo," Amesema Kibwengo.


Amesema pia wamefanya uchambuzi wa mifumo ya utendaji na utoaji huduma katika maeneo ya vyama vya ushirika, fedha, michezo na maliasili  ambapo lengo la uchambuzi huo ni kubaini mianya ya rushwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...