Na Amiri kilagalila,Njombe

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Takukuru mkoa wa Njombe imefanikiwa kurejesha fedha za riba ya ziada kiasi cha shilingi Milioni 5 iliyotozwa kwa mwalimu mstaafu wa shule ya msingi na moja ya taasisi ya kifedha zinazotoa mikopo kwa wananchi kwa kukiuka sheria.

Hayo yamebainishwa na mkuu wa Takukuru mkoa wa Njombe Bi.Domina Mukama wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo katika robo ya April-Juni 2020

“Takukuru mkoa wa Njombe tumeshaanza kulifanyia kazi na tumeweza kurejesha fedha za riba ya ziada kiasi cha Shilingi Milioni 5 iliyotozwa kwa mwalimu mstaafu wa shule ya msingi”alisema Mukama

Awali mkuu wa Takukuru mkoa wa Njombe alisema kumejitokeza na taasisi za kifedha zinazotoa mikopo huku taasisi nyingine zikikiuka taratibu za kisheria katika utoaji wa mikopo na ufanyaji wa biashara ya fedha.

“Baadhi ya taasisi hizi zimekuwa zikikiuka sheria,taratibu na kanauni zilizowekwa kuendesha shughuli zao kwa kuwatoza riba kubwa wananchi zaidi ya ile waliyokubalina na kuwapokonya kadi zao za benki.Kitendo hiki ni kosa la na wakopeshaji hao wananpaswa kuchukuliwa hatua za kisheria”aliongeza Mukama

Hata hivyo ameto wito kwa taasisi za kifedha mkoani Njombe kuzingatia sheria,kanuni na taratibu za uendeshaji wa shughuli zao pamoja na kuwasihi wananchi kutoa taarifa TAKUKURU mapema yanapojitokeza mambo yaliyo kinyume na sheria au yasiyo ya kawaida ili hatua stahiki zichukuliwe.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...