Na
Amiri kilagalila,Njombe
Kampuni
ya uchimbaji wa madini ya makaa ya mawe Tancoal imetekekeleza ombi la waziri wa
madini Doto Biteko kwa kukabidhi tani 30 za makaa ya mawe,juu ya kumsaidia mzee
Reuben Mtitu maarufu kwa jina la mzee Kisangani wa Kijiji cha Mkiu wilayani
Ludewa Mkoani Njombe kutokana na changamoto ya upatikanaji wa makaa hayo kwa
ajili ya kuyeyusha chuma ili kutengeneza bidhaa zake kama visu na nyundo.
Akizungumza
wakati akikabidhi tani 30 za Lori la makaa yam awe,afisa utawala na mahusiano ya hamii wa kampuni ya Tancoal
Richard Nditi,amesema kwa vikao tofauti kwa kushirikiana na waziri wa madini
Doto Biteko wamepanga kumfikishia mzee huyo tani 60 kwa mwaka.
“Kampuni
imepanga kukuletea tani 60 kwa mwaka kwa hiyo tumeleta tani hizi 30 utazitumia
na wakati wowote tutaleta tani 30 nyingine ili kukunga mkono kwenye shughuli
zako hizi,na tunaamini kwa kukuwezesha nishati hii unaweza ukaongeza wigo wa
shughuli zako na kuongeza fursa za ajira kwa vijana katika eneo hili la
Ludewa”alisema Richard
Maganga
Laurence ni afisa mradi wa shirika la taifa la Maendeleo (NDC) ambaye pia ni
mwakilishi wa shirika kwenye mradi wa makaa yam awe Ngaka (Tancoal),kwa niaba
ya mkurugenzi wa shirika la maendeleo ya taifa amesema wamekabidhi tani 30 kwa
sasa na baadaye tani nyingine 30 kukamilisha tani 60 kwa kuwa serikali kwa
kushirikiana na Tancoal ni kuwasaidia wajasiriamali wadogo.
“Mikakati
iliyopo mojawapo ni kudumisha mahusiano na jamii,hivyo lilivyokuja ombi la mzee
Mtitu kwa Tancoal na NDC kwa pamoja tumeona tulete tani hizi,na vile vile
ninampongeza mzee mtitu alivyopata maono ya kuanzisha kiwanda hiki”alisema
Maganga Laurence
Reuben
Mtitu maarufu kama Mzee Kisangani anayemiliki mradi wa kiwanda kidogo cha
kutengeneza bidhaa zinazotokana na chuma,ameishukuru serikali na kampuni hiyo
kwa kuwa mkaa ndio hitaji kubwa kwake na ameahidi kuingia katika utekelezaji
kwa nguvu zote.
“Madhumuni
ya waziri alivyotutembelea ni kuona mradi unakua endelevu,napenda
kuwahakikishia Tancoal kwa kushirikiana na serikali sisi tunaingia kwenye
utekeleaji wa kuzalisha chuma ili tuweze kujikimu sisi wenyewe lakini pia kwa
manufaa ya taifa”alisema Mzee Reuben Mtitu
Nicolaus
Mgaya ni Diwani wa kata ya Lubonde na Verdiana Mnzeru ni mtendaji wa kata hiyo
wameishukuru pia serikali kwa kumuwezesha mzee huyo kwa kuwa shughuli
anazofanya ni kwa manufaa ya kata,wilaya na taifa kwa ujumla hivyo wememtaka
mzee Kisangani kuutumia vema mkaa huo ipasavyo pamoja na kuwezesha ajira kwa
vijana.
Tancoal
na Ndc wamefikisha mkaa huo kutokana ombi la waziri Doto Biteko alipofika machi
14 2020 wilayani Ludewa mkoani Njombe alipotembelea mradi wa kiwanda cha
kuzalisha zana mbali mbali zinazotokana
na madini ya chuma kinachomilikiwa na Mzee Kisangani na kukutana na changamoto
ya makaa ya mawe anayokumbana nayo mzee huyo hatu iliyokuwa ikimlazimu kufanya
kazi wakati tu anapopata malighafi hiyo kwa kuvizia na kuokota makaa
yanayodondoshwa barabarani wakati yakisafirishwa.
Makaa ya mawe yakimwaga tayari kukabidhiwa kwa mzee Kisangani ili kumuwezesha katika kazi zake za uyeyushaji wa chuma.
Richard Nditi afisa utawala na mahusiano wa kampuni ya Tancoal akizungumza namna walivyopokea taarifa za mzee Kisangani anavyojituma katika ubunifu wake wa utengenezaji wa zana zinazotokana na chuma na kumkabidhi tani 30 za makaa.
Maganga Laurence ni afisa mradi wa shirika la taifa la Maendeleo (NDC) akizungumzaushirikiano ulipo baina ya NDC na Tancoal na kumuomba mzee Kisangani kuendelea najuhudi zake za uhunzi.
Afisa utawala wa Tancoal Richard Nditi akizungumza na mzee Kisangani katika mradi wake wa uyeyusahji chum
Eneo la mradi wa uyeyushaji chuma linalomilikiwa na Mzee mtitu lililopo kijiji cha Mkiu kata ya Lubonde wilayani Ludewa mkoani Njombe. Wageni kutoka Tancoal na NDC wakinawa mikono kuepuka maambukizi ya ugonjwa wa Corona mara baada ya kufika kwenye mradi wa uyeyushaji chuma unaomilikiwa na mzee Kisangani

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...