TEKNOLOJIA  inaendelea kukua kwa kasi katika uzalishaji wa simu janja na Infinix Imethibitisha hili kupitia toleo jipya la Infinix S5pro iliingia sokoni mapema mwezi huu. Infinix S5pro ni simu ya kwanza kwa kampuni ya Infinix kuwa na teknlojia ya pop up camera.

 Fahamu mengi zaidi ya Infinix S5pro;
Simu hizi zina RAM zenye ukubwa tofauti wa 4GB na 6GB hivyo itakuwezesha kufungua programu au kufanya mambo mbalimbali kwa wakati mmoja bila kukwama kwama, na uwezo wake wa kuhifadhi taarifa (video, picha, miziki, faili) ni 64GB na 128GB. 

Aidha, ina sehemu ya kuweka memory card kwa ajili ya kuiongezea uwezo wa kuhifadhi taarifa.
Kwa wale wanaopenda simu zenye kioo kikubwa na chenye ubora simu hii yenye uzito wa gramu 195 ni kwa ajili yao kwani kioo chake (IPS LCD) kina ukubwa wa inchi 6.53" chenye ubora wa 1080p. 

Kamera yake ya mbele (selfie camera) yenye 40MP ni ya kipekee zaidi ambapo hutokezea juu ya simu pale unapotaka kupiga picha na ukimaliza inarudi kujificha ndani ya simu, (mechanical pop-up piece) hii inakuwezesha kupata picha zenye ubora zaidi.

Wale wapiga picha, simu hii ina kamera 3 za nyuma ambapo kamera ya kwanza ina 48MP (f/1.8 lens), kamera nyingine ina 2MP ambayo hii ni sensor kwa ajili ya picha za karibu (potraits) ambazo huonesha hadi sehemu ya mabega. Kamera ya mwisho (QVGA) ni maalum kwa ajili ya kuweka sawa mwanga wakati wa upigaji picha. Pia inauwezo wa kurekodi video zenye ubora na muonekano ang'avu wa hadi 1080p. Yote haya ni kuhakikisha wewe mtumiaji unapata kilicho bora zaidi.

Uwezo wa betri ya simu hii ni 4,000 mAh ambayo inaweza kukaa zaidi ya siku moja bila kuichaji. Simu hii ina mfumo endeshi (OS) Android 10, na utaweza kuuboresha kadiri maboresho yatakavyotoka. 

Katika kuhakikisha kuwa unapata habari mahali popote ulipo, ndani ya simu kuna programu ya redio (FM Radio). Jingine ni kwamba tumeimarisha usalama wa taarifa zako kwani utaweza kuifunga simu yako kwa kutumia alama za kidole.

Wajanja wanatumia vyenye ubora wa kipekee, tembelea sasa duka letu la Infinix lililopo karibu nawe uwe wa kwanza kujipatia simu hii. Ukikosa utaambia nini watu?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...