Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na waumini wa Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania, Usharika wa Bariadi Mjini (hawapo pichani), wakati
alipofika kanisani hapo kutoa salamu za Pasaka kwa waumini hao leo
Aprili 12, 2020 kushoto ni Mchungaji wa Kanisa hilo, Greyson Kinyaha na
kulia ni Mchungaji Sarah Kimaro.

aadhi ya waumini wa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Usharika wa Bariadi Mjini wakimsikiliza
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka wakati alipofika kanisani
hapo kutoa salamu za Pasaka kwa waumini hao leo Aprili 12, 2020.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka akipokea ekaristi takatifu katika misa takatifu Kanisa
Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Bariadi Mjini, wakati aliposhiriki
katika misa hiyo na kutoa salamu za pasaka kwa waumini wa Kanisa hilo
waumini hao leo Aprili 12, 2020.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na waumini wa Kanisa la Africa Inland
Church of Tanzania(AICT) Bariadi Mjini wakati alipofika kanisani hapo
kutoa salamu za Pasaka kwa waumini hao leo Aprili 12, 2020.

Paroko Msaidizi wa Parokia ya
Mtakatifu John Bariadi Mjini,Peter Mkunya akitoa mahubisri ya neno la
Mungu katika misa Takatifu leo Aprili 12, 2020.

Waimbaji wa Kwaya ya Uinjilisti
katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Usharika wa Bariadi
Mjini wakiimba wakati wa ibada ya kwanza leo Aprili 12, 2020
kuadhimisha Siku ya Pasaka ambapo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony
Mtaka ameshiriki katika ibada hiyo na kutoa salamu za pasaka kwa
waumini na wananchi.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka akinawa mikono kwa maji tiririka na sabuni mara baada
ya kuwasili katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT)
Bariadi Mjini ambapo ameshiriki ibada ya Pasaka na kutoa salamu za
Pasaka za Mkoa leo Aprili 12, 2020 kwa waumini wa Kanisa hilo.

Waimbaji wa Kwaya kutoka Kanisa la
Africa Inland Church of Tanzania(AICT) Bariadi Mjini wakiimba wakati wa
ibada leo Aprili 12, 2020 kuadhimisha Siku ya Pasaka ambapo Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ameshiriki katika ibada hiyo na
kutoa salamu za pasaka za mkoa kwa waumini wa kanisa hilo.

Mchungaji wa Kanisa la Africa
Inland Church of Tanzania(AICT) Bariadi Mjini, Amosi Ndaki akitoa
mahubiri ya neno la Mungu wakati wa ibada leo Aprili 12, 2020
kuadhimisha Siku ya Pasaka ambapo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony
Mtaka ameshiriki katika ibada hiyo na kutoa salamu za pasaka za mkoa
kwa waumini wa kanisa hilo.

Kwaya ya Mtakatifu Johh kutoka
Parokia ya Mtakatifu John Bariadi Mjini wakiimba wakati wa misa
takatifu leo Aprili 12, 2020 kuadhimisha Siku ya Pasaka ambapo Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ameshiriki katika misa hiyo na kutoa
salamu za pasaka za mkoa kwa waumini wa kanisa hilo.

Baadhi ya
wanakwaya na Waumini wa Kanisa la Mtakatifu Luka Mjini Bariadi
wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati
akitoa salamu za Pasaka za Mkoa kwa waumini wa kanisa hilo leo Aprili
12, 2020.
……………………………………………………………………………………………
Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka leo ameshiriki ibada ya Pasaka katika
makanisa tofauti mjini Bariadi na kuwasisitiza waumini na wananchi wote
wa Mkoa wa Simiyu kutulia, kuepuka safari zisizo za lazima na kuendelea
kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona kwa
kuzingatia maelekezo yanayotolewa na Serikali.
Mtaka
ameyasema hayo kwa nyakati tofauti wakati akitoa salamu za Pasaka za
Mkoa aliposhiriki ibada katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu
John, Parokia ya Mtakatifu Luka, Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT) Bariadi Mjini na Kanisa la Africa Inland Church of
Tanzania (AICT) leo Aprili 12, 2020.
“Nimeona watu
wananawa mikono utaratibu huu usiishie kwenye nyumba za ibada na maeneo
ya kutolea huduma, uende mpaka nyumbani,tunapokuwa kwenye nyumba za
ibada pia tuzingatie umbali katika ukaaji wetu na wakati wa kupokea
huduma za kiroho: pasaka hii tutulie majumbani tuepuke safari zisizo
lazima na tufuate maelekezo ya Serikali.” alisema Mtaka.
Aidha, pamoja na
kuwasisitiza wananchi kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima Mtaka ametoa
wito kwa jamii kuona namna ya kuwasaidia zaidi wazee, watoto na watu
wenye magonjwa yasiyoambukiza kama kisukari na shinikizo la damu kuepuka
zaidi mikusanyiko hiyo ili kuwaondolea hatari ya kupata maambukizi
kutokana na hali ya kinga zao za mwili.
Katika hatua
nyingine Mtaka amewataka wazazi kuwasimamia watoto wao kujisomea kwa
bidii kipindi hiki ambacho shule zimefungwa kutokana na tahadhari ya
maambukizi ya Virusi vya Corona hususani wale wa madarasa ya Mitihani ya
Kitaifa kwa kuwa mitihani hiyo bado ipo na itafanyika.
Sambamba na hayo
Mtaka amewaasa wananchi wa Mkoa wa Simiyu kutunza chakula ambacho
kimepatikana mwaka huu na kutokiuza kwa matumizi ambayo si ya lazima
hususani katika kipindi hiki ambacho chakula kinauzwa kwa bei ya chini
huku akiwasisitiza kujiunga na Bima ya Afya na Mfuko wa Afya ya Jamii
ili waweze kupata unafuu katika huduma za matibabu.
Kwa upande wao
viongozi wa makanisa akiwemo Paroko Msaidizi wa Parokia ya Mtakatifu
John, Peter Mkunya, Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Luka, Martine Jilala,
Mchungaji wa KKKT Bariadi, Greyson Kinyaha na Mchungaji wa AICT, Amosi
Ndaki wamesema wametumia Maadhimisho ya Kufufuka kwa Yesu Kristo(Pasaka)
kuliombea Taifa ili Mungu aliponye na Janga la Corona na kuendelea
kuwakumbusha waumini kuzingatia maelekezo ya viongozi wa Serikali na
wataalam wa afya.
Koga Mihama na
George Lyimo ni miongoni mwa waumini waliohudhuria ibada ya pasaka
wameishukuru Serikali kwa jitihada zinazoendelea kuchukuliwa kujikinga
na Maambukizi ya CORONA huku wakitoa wito kwa wananchi wote kufuata
maelekezo yanayotolewa na Serikali ili Maambukizi ya Virusi vya Corona
yaishe nchini Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...