Viongozi wa dini nchini wamehimizwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa wanaisaidia Serikali,katika kuhamasisha jamii kuhusiana na kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona vinavyosababisha Ugonjwa wa Covid-19.

Akizungumza na Vyombo vya habari Msemaji wa Taasisi ya dini ya Kiislaamu ya TWARIQA Qadiria,Jalailania Arrasziqia Tanzania Shekhe Haruna Hussein alisema viongozi wa dini Wana nafasi kubwa Sana katika kusaidia mapambano haya ya Virusi vya Corona,kwa kuhakikisha kuwa katika makanisa na misikiti wanahimiza waumini kufanya yale yote ambayo wizara ya afya imekuwa ikitoa Kama tahadhari.

Alisema kuwa dhamana kubwa ya Viongozi hao iwasaidie wananchi na taifa katika kulifikisha sehemu salama,kwa kuliombea pamoja na kuendelea kuchukua tahadhari."viongozi wa dini tuna dhamana kubwa Sana na tunatakiwa tutenge muda japo dakika kumi tu kwaajili ya kumuomba Mungu atunusuru na tutubu hakuna toba ya kweli Mungu ataikataa tuombe rehma zake na atuondoshee gonjwa hili la Corona."alisema Haruna.

Alisema kuwa ili kupambana na janga Hili ni lazima kuhakikisha kuwa kila mmoja anatoa mchango wake ili kuokoa kizazi hiki na kijacho.Aidha aliwataka watanzania wanaoishi mipakani kuchukua tahadhari zaidi kutokana na mwingiliano uliopo ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa hata Kama ni ndugu zao wanaingia nchini kinyume Cha sheria kwa kuwa janga la Covid-19 ni la watanzania wote.

Alisema kuwa wakati umefika Sasa wa kuachia Serikali pekee kutoa taarifa Mbali Mbali Kama ilivyoelekezwa na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa taarifa zote zitatolewa na waziri wa Afya,Ummy Mwalimu.

Alisema kauli ya raisi ni ya kuheshimiwa kwa kuwa ikiwa kila mtu atatoa taarifa Basi ni wazi kuwa watanzania watachanganyikiwa na kushindwa kutii maalekezo ya msingi.

Naye Shekhe Idd Ngela alisema kuwa wakati dunia ikiweweseka na Gonjwa Hilo watanzania wanapaswa kurejea kwa Mungu na kuhakikisha kuwa wanajitathimini Ni Jambo gani Wanaweza kufanya ili kuokoa wengine.

Hata hivyo aliwataka watanzania kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima ili kujilinda na maambukizi ya Ugonjwa wa Covid-19.Taasisi ya TWARIQA ni chombo Cha Kiislaamu ambacho kilianzishwa miaka themenini iliyopita,Makao Makuu yake yakiwa Mkoani Kilimanjaro lengo likiwa Ni kuwawezesha waislam kiimani na kuhakikisha kuwa wanashiriki katika Mambo Mbali Mbali ya kusaidia jamii.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...