Na Woinde Shizza,ARUSHA

WADAU wa Maendeleo Mkoa wa Arusha wameunga mkono juhudi za Serikali dhidi ya mapambano ya ugonjwa hatari wa Covid-19 kwa kutoka misaada mbalimbali kama njia mojawapo ya kukabiliana maambukizo ya virusi vya Corona.

Misaada hiyo imetolewa na kampuni ya vinywaji vikali ya Mega Beverage ya jijini hapa kuwa ambapo imetoa lita 2500 za vitakasa mikono pamoja na madumu 50 ya kunawia maji yanayotiririka vyenye thamani ya sh,milioni 46.

Wadau wengine waliojitokeza kuchangia mapambano hayo ni kampuni ya usafirishaji wa Magari ya Simba Tracking waliochangia Sh.milioni 10 wakati Kampuni ya magari ya Hanspoll ikichangia Sh.milioni 10 fedha ambazo zitatumika kukarabati jengo la kuhifadhia wagonjwa wa Korona.

Akizungumza baada ya kupokea misaada hiyo Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema virusi vya corona ni hatari na vinaua na kuwataka wakazi wa mkoa huo kuchukua tahadhari kwani mpaka sasa ugonjwa huo hauna tiba .

Gambo amesema katika mapambano ya ugonjwa huo Serikali mkoa wa Arusha imepanga kutumia Sh.milioni 195 milioni kwa ajili ya kukarabati jengo la karantini lililopo katika hospitali ya mkoa ya Mt.Meru ambapo mpaka sasa tayari zimeshakusanywa Sh.milioni 95 kwa ajili ya ukarabati huo.


Pia amesema kaatika mgawanyo wa vifaa vilivyotolewa na wadau hao wa maendeleo lita 100 wamekabidhiwa jeshi la magereza mkoani Arusha, jeshi la polisi lita 100 na nyingine zitapelekwa katika vituo vya mabasi na vya afya.

Amesisitiza Serikali mkoani Arusha inawashikiliwa baadhi ya watu ambao wanadaiwa kuingia nchini kupitia njia za panya kupitia mpaka wa Namanga ambao alidai ni mkubwa sana.

Akikabidhi misaada hiyo Meneja wa Kampuni ya Mega Beverages, Christopher Ndossi amesema wanaunga mkono juhudi za Serikali katika kupambana na ugonjwa huo wao kama wadau wa maendeleo.

Ndosi amesema katika kuimarisha uchumi wa nchi wao kama wadau wa Maendeleo wana jukumu la kuhakikisha wanashirikiana na serikali kama njia mojawapo ya kupambana na ugonjwa huo hatari.

Wakati huo huo Mkurugenzi wa Kampuni ya Hans Paul , Satbir Hanspaul pamoja na mkurugenzi wa kampuni ya Simba Truck ,Raji Grewal kwa pamoja wamesema wao kama wadau wa maendeleo mkoani Arusha wameamua kuchangia fedha hizo kwa ajili ya ukarabati wa jengo la karantini .

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Wesson Sichalwe amesema mahitaji ya vifaa vya kukabili Korona bado ni makubwa na kuwataka wadau wengine kuendelea kuchangia has a vifaa kama sabuni,glovu, barakoa na vitakasa mikono.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...