Na Amiri kilagalila, Njombe
KUTOKANA na elimu ya namna ya kujikinga na ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayotokana na virusi vya Corona (COVID-19) kutowafikia vyema wananchi waishio maeneo ya vijijini wadau mbalimbali wa maendeleo mkoani Njombe wameanza zoezi la kwenda kutoa elimu kwa wananchi juu ya kujikinga na ugonjwa huo.
Miongoni mwa wadau hao ni Johson Mgimba na Lawi Mnyanga ambao wamefika katika kata ya Madilu wilayani Ludewa mkoani Njombe na kutoa elimu kwa wananchi mbalimbali kupitia maeneo ya ibada ambapo wamewataka wananchi kufuatilia vyombo mbalimbali ili kufuatilia taarifa za wataalam wa afya ili kujikinga na virusi vya Corona
Baadhi ya wananchi waliofikiwa na elimu hiyo wamewashukuru wadau wa maendeleo wakiwemo vijana kutoka kata ya Madilu huku wakiwa tayari kukabiliana na ugonjwa huo kwa kufuata kanuni za afya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...