
Wakazi wa Kata ya Osunyai jijini Arusha wakinawa mikono kujikinga dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa corona kabla ya kuingia kwenye vyumba kujiaandikisha na kubadilisha taarifa zao katika mpango wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) kuboresha daftari la kudumu la wapigakura katika mikoa 12 ya mwanzo kabla ya uchaguzi mkuu Oktoba 2020.

Msimamizi Msaidizi wa uchaguzi Arusha Mjini,Dk Maulid Madeni akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mwenendo wa uandikishaji wapigakura jijini Arusha.

Wananchi wakijiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapigakura katika kituo kilichopo Shule ya Msingi Osunyai jijini Arusha.

Wananchi wakijiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapigakura katika kituo kilichopo Shule ya Msingi Osunyai jijini Arusha.

Mkazi wa Kata ya Elerai jijini Arusha akiangalia jina lake ili akamilishe uandikishaji katika daftari la kudumu la wapigakura utaratibu unaosimamiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Msimamizi wa Uchaguzi katika halmashauri ya Jiji la Arusha,Msena Bina akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mwenendo wa uandikishaji wapigakura jijini Arusha.

Wakazi wa Kata ya Osunyai jijini Arusha wakiwa wamejipanga mistari kwa kuzingatia maelekezo ya wataalamu wa afya ili kujikinga dhidi ya ugonjwa wa corona wakati wa kujiaandikisha na kubadilisha taarifa zao katika daftari la kudumu la wapigakura unaoratibiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...