Felista Giyam mhasibu wa kikundi cha hamasa ameiomba serikali kuona uwezekano wa kutafuta masoko kwa mazao ya wakulima kwani wamekuwa wakilima kwa muda mrefu lakini wanakosa masoko hivyo kuwakatisha tamaa licha ya kukiri kuwa wamekuwa na faida kwa wastani japo soko linaendelea kuwa kikwazo licha ya kwamba pia wakulima wamekuwa wakitumia gharama kubwa katika pembejeo za kilimo

Anna Iselu mbaye ni mhasibu wa kikundi cha wanawake na vijana cha Gosanga anasema mradi huo utawafanya kutokuonekana mizigo ndani ya familia na kwa jamii kwa ujumla na kuleta mtazamo mwingine mpya na chanya miongoni mwa jamii
Albert Masuja muwakilishi kutoka shirika la UCRT wamewawezesha jumla ya wanawake 45 katika Kijiji Mureru kata ya Balangdalalu wilayani hanang kuanzisha mradi wa kilimo cha umwagiliaji ili kuondokana na utegemezi wa asilimia 100 kwa wanaume zao.
Baadhi ya wakinanana wanufaika wa mradi huo wakibadilishana mawazo wakiwa sahambani kukagua mazao yanaendeleaje

Donath Fungu Meneja wa miradi ya Oxfam kanda ya kaskazini akitoa ufafafanuzi wa mradi huo unavyoendelea kwa sasa
Charles Kidaguwi mmoja wa wanaume walioshiriki katika mradi huo wa wanawake na vijana kwaajili ya kujikwamua kiuchumi katika kijiji cha Mureru wilayani Hanang' mkoa wa Manyara.

Anna Iselu mbaye ni mhasibu wa kikundi cha wanawake na vijana cha Gosanga akikagua mazao katika shamba la mradi wa wanawake na baadhi ya wanaume waliojiunga katika vikundi hivyo
Charles Kidaguwi ambaye ni mmoja wa wanakikundi na mlizi wa shamba la mradi akifurahia jambo

Baadhi ya wanakikundi wakitoka kukagua shamba la mradi wa mahidi waliowezeshwa na Oxfam pamoja na Acrt amabao wanatarajia kuvuna zaidi ya magunia 100-150 kwa mujibu wa wataalam wa kilimo.


Na Vero Ignatus,Manyara.

Katika kuhakikisha kuwa jamii inajikwamua kiuchumi shirika la Oxfam Tanzania kwa kushirikiana na Ujamaa community resources (UCRT wamewawezesha jumla ya wanawake 45 katika Kijiji
Mureru kata ya Balangdalalu wilayani hanang kuanzisha mradi wa kilimo cha
umwagiliaji ili kuondokana na utegemezi wa asilimia 100 kwa wanaume zao.

Wakieleza manufaa ya mradi huo kwao wanawake hao kwa nyakati tofauti wamesemakuwa mradi huo utawafanya kutokuonekana mizigo ndani ya familia na kwa jamii kwa ujumla na kuleta mtazamo mwingine mpya na chanya miongoni mwa jamii wilayani hapo kufuatia jamii ziishio Hanang kutokumpa nafasi mwanamke hivyo kuendelea kuwa na uchumi tegemezi kwa miongo yote.

“Huu mradi kwakweli kwanza tunawashukuru Oxfam na Ucrt kwa kutuletea mradi huu unajua huu mradi utatukwamua sana kiuchumi na hata kusaidia baadhi ya majukum kwenye Familia”alisema Felista Giyam ambaye ni mhasibu wa kikundi cha wanawake hao.

Ameongeza kuwa pamoja na mradi huu kulenga wanawake ndani yake kuna wanaume ambao tumeamua  kushirikiana nao kwani sisi tunaamini “hapa ndani ya mradi kuna wanaume 12 kati yet una hapo tumeamua sana katika umoja.kushirikiana kwa sababu ni mwanzo” Alisema Felista

Mmoja ya wanakikundi mwingine Anna Iselu pia kwa niaba ya wanawake hao na kikundi hicho cha muungano ameiomba serikali kuona uwezekano wa kutafuta masoko kwa mazao ya wakulima kwani wamekuwa wakilima kwa muda mrefu lakini wanakosa masoko hivyo kuwakatisha tamaa licha ya kukiri kuwa wamekuwa na faida kwa wastani japo soko linaendelea kuwa kikwazo licha ya kwamba pia wakulima wamekuwa wakitumia gharama kubwa katika pembejeo za kilimo.

“Unajua hapa tunatumia gharama kubwa wakati wa kununua pembejeo lakini tunakosa masoko jambo hili linaturudisha nyuma kwakweli serikali iangalie namna ya kuwawezesha wakulima hasa sisi wanawake ambao tumeamua kujiingiza katika kilimo” Alisema Anna Iselu mmoja ya wanakikundi.

Charles Kidaguwi ni kati ya wanaume ambao wameshiriki katika mradi huo amesema kwake una manufaa makubwa kwani utamsaidia kuwajibika vyema katika familia zaidi tofauti na awali kwani kwake ni chanzo kimojawapo cha mapatao ,pia kwa upande wa mwanamke itamsaidia kujikwamua kiuchumi,na kutoa mchango katika familia tofauti na awali walikuwa wanakaa nyumbani pekee.

Kwasababu sikuzote familia inalaliaga upande wangu lakini kama mama amepata mradi huu wa kilimo basi na mimi nitapata msaada mkubwa alisema Chalrles Kidaguwi kutoka Kijiji cha Mureru wilaya ya Hanang’ mkoa wa Manyara

 Kwa upande wake Donath Fungu Meneja wa miradi ya Oxfam kanda ya kaskazini amesema mradi huo wanaufanya kwa kuwashirikisha wanawake na vijana lengo likiwa ni kuwajengea wanawake uwezo kiuchumi kipato kiuchumi kwani mwanamke anajishughulisha na mambo mengi ila jamii haimtambui

Ukimuwezesha mwanamke umeiwezesha familia ,jamii na Taifa kwa ujumla hivyo Oxfam Tanzania nzima mdau wetu mkubwa tunaesgughulika nae ni mwananmke,kitendo chake cha kutambulika kinatokana na nguvu yake ya kiuchumi kuwa ndogo tunaamini kwamba atakapopata nafasi ya kuinuka kiuchumi

Fungu amesema mwanamke atakapopata nguvu ya kuinuka
kiuchumi atapata nafasi ya kufanya maamuzi katika ngazi ya kifamilia Kijiji
hadi ngazi ya kitaifa,amesema pamoja na hayo pia wanawapatia mafunzo ya uongozi ,kujiamini ambapo hadi sasa wamefikia hatua kubwa

Amesema hapo awali katika wilaya hiyo mwanamke alikuwa haruhusiwi kusimamam mbele ya jamii na kuzungumza chochote ila baada ya mafunzo waliyowapatia wameweza kujiamini na baadhi yao wameweza kugombea nafasi mbalimbali katika ngazi za vijiji,kuwepokatika na kamati za vijiji na nafasi mbalimbali muhimu.

Naye Mratibu wa Mradi kutoka UCRT Masuja alisema kuwa malengo ni kumpa mwanamke  fursa ili aweze kuboresha Maisha yake kiuchumi ambapo wameweza kuwaweka katika vikundi ili waweze kufanya kazi kwa pamoja na kuleta ufanisi Zaidi

Amesema katika kushirikiana na Oxfam wameweza kutoa
nafasi kwa mwanamke kumiliki ardhi wapatao 365 pamoja na kuwapatia hati miliki,pia wameweza kuwapatia wakinamama wa kikundi cha hamasa ng’ombe wapatao 9 na sasa wamepo 18 lengo ni kuwakwamua kiuchumi pamoja na vijana kujitambua na kujiandaa kuja kuwa na familia baadae.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...