Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka akizungumza na waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato
Bariadi Mjini, Aprili 18, 2020 ambapo ameshiriki katika ibada ambayo
waumini hao wameitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli kwa Watanzania wote kuingia katika maombi
ya siku tatu ( Aprili 17-19, 2020) kuliombea Taifa ili Mungu aliponye na
janga la Corona.

Baadhi ya Wazee wa Kanisa wa
Kanisa la SDA Bariadi mjini wakiwaongoza waumini wa kanisa hilo katika
maombi maalum ya kuliombea Taifa, yaliyofanyika katika ibada Aprili 18,
2020 kuitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli kwa Watanzania wote kuingia katika maombi ya siku
tatu ( Aprili 17-19, 2020) kuliombea Taifa ili Mungu aliponye na janga
la Corona.(mwenye Tai wa tatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka).

Baadhi ya waumini wa Kanisa la
Waadventista Wasabato Bariadi Mjini, Aprili 18, 2020 wakimsikiliza Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ambapo ameshiriki ibada ambayo
waumini hao wameitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Watanzania wote kuingia katika maombi
ya siku tatu ( Aprili 17-19, 2020) kuliombea Taifa ili Mungu aliponye
na janga la Corona

Kwaya ya Kanisa la Waadventista
Wasabato Bariadi Mjini wakiimba katika ibada ya Aprili 18, 2020 ambayo
waumini wa kanisa hilo pia wameitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Watanzania wote
kuingia katika maombi ya siku tatu ( Aprili 17-19, 2020) kuliombea Taifa
ili Mungu aliponye na janga la Corona.

Mchungaji wa Kanisa la
Waadventista Wasabato Bariadi Mjini, Marco Mlingwa akiwaongoza waumini
wa kanisa hilo(hawapo pichani) katika maombi maalum ya kuliombea Taifa,
yaliyofanyika katika ibada Aprili 18, 2020 kuitikia wito wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa
Watanzania wote kuingia katika maombi ya siku tatu ( Aprili 17-19, 2020)
kuliombea Taifa ili Mungu aliponye na janga la Corona.(wa pili kushoto
ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka).

Mmoja wa waimbaji wa kwaya ya
Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi Mjini akipuliza dawa katika
vipaza sauti kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya
Corona, kwenye ibada ambayo waumini wa Kanisa hilo wameitikia wito wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
kwa Watanzania wote kuingia katika maombi ya siku tatu ( Aprili 17-19,
2020) kuliombea Taifa ili Mungu aliponye na janga la Corona.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka (kushoto) na Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wasabato
Bariadi Mjini, Marco Mlingwa wakiwa katika maombi kwenye ibada ambayo
waumini wa Kanisa hilo wameitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Watanzania wote kuingia
katika maombi ya siku tatu ( Aprili 17-19, 2020) kuliombea Taifa ili
Mungu aliponye na janga la Corona.

Baadhi ya waumini wa Kanisa la
Waadventista Wasabato Bariadi Mjini, Aprili 18, 2020 wakimsikiliza Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ambapo ameshiriki ibada ambayo
waumini hao wameitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Watanzania wote kuingia katika maombi
ya siku tatu ( Aprili 17-19, 2020) kuliombea Taifa ili Mungu aliponye na
janga la Corona.
………………………………………………………………………………………………
Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema kuwa jumla ya watu 34 kati ya watu
120 waliokuwa kwenye uangalizi maalum (Karantini) mkoani Simiyu
wameruhusiwa mara baada ya kupimwa na kukutwa hawana maambukizi ya
Virusi vya Corona vinavyosababisha homa kali ya mapafu (COVID-19).
Mtaka
ameyasema hayo Aprili 18, 2020 wakati akizungumza na waumini wa Kanisa
la Waadventista Wasabato (SDA) Bariadi Mjini, ambao wameitikia wito wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
kwa Watanzania kuingia katika maombi ya siku tatu (Aprili 17-19, 2020)
kuliombea Taifa ili Mungu aliponye na janga la Corona.
“Tulikuwa na watu
120 waliokuwa chini ya uangalizi ambao pia wamekuwa wakipata elimu
kuhusu maambukizi ya virusi vya Corona ili wakitoka wakawe msaada kwa
familia zao; mpaka sasa watu 34 wameruhusiwa baada ya kupimwa na
kuthibitika kwamba hawana maambukizi ya Corona, sisi kama mkoa
tunaendelea kuchukua tahadhari zote,”alisema Mtaka.
Ameongeza kuwa
waliowekwa karantini ni pamoja na wanaofanya biashara nchi jirani ambao
waliomba wenyewe ili wajitenge na familia zao; pia wapo baadhi ambao
familia ziliomba Serikali iwaweke kutokana na kujua kuwa wametoka nchi
zenye maambukizi kwa hofu ya kupeleka maambukizi kwa familia zao ikiwa
itatokea wameambukizwa virusi vya Corona.
Aidha, Mtaka
amesema kuwa mpaka sasa mkoa wa Simiyu hauna mtu mwenye maambukizi ya
Virusi vya Corona na kutoa wito kwa wananchi kuendelea kuchukua
tahadhari huku wakimuomba Mungu bila kukoma ili aliponye Taifa na janga
la kidunia la ugonjwa wa COVID 19.
Katika hatua
nyingine Mtaka amewahimiza wazazi kuwasimamia watoto wao na kuhakikisha
wanajisomea wakiwa nyumbani huku akiwaasa kutunza chakula na kuepuka
kuuza mazao pasipo na ulazima wa kufanya hivyo.
Mchungaji wa
Kanisa la SDA Bariadi Mjini, Marco Mlingwa amesema Kanisa hilo limepokea
maelekezo ya Serikali na linaungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuliombea Taifa Mungu aliponye
na janga la Corona.
Kwa upande wao
waumini wa Kanisa la SDA Bariadi Mjini wamemshukuru Mhe. Rais kuruhusu
ibada kufanyika kwa kuzingatia maelekezo ya watalaam wa afya na
kubainisha kuwa wataendelea kumuomba Mungu aliepushe Taifa na Corona
wakiamini kuwa Mungu atasikia wakiomba kwa imani na kwa bidii.
“Tunamshukuru
Mhe. Rais kuruhusu ibada kuendelea kufanyika huku tukichukua tahadhari,
sisi Wakristo tunaamini watu tukiomba kwa bidii Mungu anasikia maombi,
hivyo tukikutana na kuomba kwa bidii Mungu atasikia na kutuokoa na
ugonjwa huu wa COVID 19,” alisema Paul Jidayi muumini SDA na Mwenyekiti
wa CCM Wilaya ya Maswa.
“Sisi kama
Wasabato tuna vipindi vyetu vya afya na kupitia vipindi hivyo
tumeshajifunza na kuchukua tahadhari dhidi ya Corona kanisani na
majumbani; pia tunaungana na Rais kuliombea Taifa tukiamini kuwa Mungu
atatusikia maana hata zamani, nchi ya Ninawi walipelekewa taarifa kuwa
wataangamizwa lakini walipomlilia Mungu aliwasikia na hawakuangamia,”
alisema Mariam Manyangu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...