Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Lubiga Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu, Buyamba Duba akiangalia kwa makini namna Mbunge wa Jimbo la Kisesa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akihakiki taarifa zake kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga
Kura katika Ofisi ya Kata ya Lubiga.
Mbunge wa Jimbo la Kisesa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akihakiki taarifa zake kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga
Kura katika Kata ya Lubiga Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu. Kulia ni Ofisa
Mwandikishaji, Joseph Mkongola.
Mbunge wa Jimbo la Kisesa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akinawa mikono kwa maji tiririka na sabuni kujikinga na
Corona kabla ya kuingia kwenye chumba maalum kwa ajili kuhakiki taarifa zake kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura katika Kata ya Lubiga Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu.
Mbunge wa Jimbo la Kisesa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akisalimia na wananchi wachache huku wakichukua tahadhari
ya kujikinga na Corona baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa Sekondari mpya ya Kata ya Isengwa Wilaya ya Meatu
==================
MBUNGE wa Kisesa, Mhe. Luhaga Mpina ameshiriki zoezi la kuhakiki taarifa kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura la Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) katika Kata ya Lubiga wilayani Meatu mkoani Simiyu.
Mpina ambaye pia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi amelazimika kufika makao makuu ya Kata kuhakiki taarifa zake baada ya baadhi ya wananchi kumjulisha kuwa taarifa zake hazijakamilika kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na Msimamzi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Lubiga.
Hivyo Waziri Mpina alifika na kufanikiwa kuhakiki taarifa zake na kupatiwa kadi mpya ya mpiga kura na kwamba sasa yuko tayari kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Katibu wa CCM Kata ya Lubiga, Buyamba Duba alimshukuru Mbunge Mpina kwa kuwahi kuhakiki taarifa zake kwani zoezi hilo lilichukua muda wa siku tatu tu.
Pia Mhe. Mpina mbali na kuhakiki taarifa zake alitumia nafasi hiyo kukagua mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Isengwa ambapo pamoja na mambo mengine alipongeza juhudi za wazazi za kufanikiwa kuanzisha shule hiyo na sasa tayari vyumba viwili vya madarasa vimeshamilika.
Diwani wa Kata ya Isengwa, Mhe. Philip Makalwe amemshukuru Mbunge Mpina kwa juhudi kubwa alizofanya za kuchangia ujenzi wa sekondari hiyo ambapo amesema utasaidia kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu kwenda hadi Sekondari ya Itinje walilokuwa wanasoma watoto kutoka kata hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...