Waziri Mkuu Mstaafu ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa Mhe Mizengo Peter Pinda akimtembeza Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) kujionea mashamba ya zabibu alipozuru katika eneo la Zuzu leo tarehe 7 Aprili 2020 Jijini Dodoma. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri Mkuu Mstaafu ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa Mhe Mizengo Peter Pinda akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) aliyemtembelea nyumbani kwake katika eneo la Zuzu leo tarehe 7 Aprili 2020 Jijini Dodoma.

Waziri Mkuu Mstaafu ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa Mhe Mizengo Peter Pinda akimtembeza Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) kujionea ujenzi wa vitalu nyumba (Green House) alipozuru katika eneo la Zuzu leo tarehe 7 Aprili 2020 Jijini Dodoma.
Waziri Mkuu Mstaafu ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa Mhe Mizengo Peter Pinda akimtembeza Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) kujionea mabwawa ya ufugaji wa samaki alipozuru katika eneo la Zuzu leo tarehe 7 Aprili 2020 Jijini Dodoma.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akionyeshwa chakula cha samaki na mwenyeji wake Waziri Mkuu Mstaafu ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa Mhe Mizengo Peter Pinda mara baada ya kumtembelea nyumbani kwake eneo la Zuzu leo tarehe 7 Aprili 2020 Jijini Dodoma.

Waziri Mkuu Mstaafu ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa Mhe Mizengo Peter Pinda akimtembeza Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) kujionea mabwawa ya ufugaji wa samaki alipozuru katika eneo la Zuzu leo tarehe 7 Aprili 2020 Jijini Dodoma.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo tarehe 7 Aprili 2020 amemtembelea Waziri Mkuu Mstaafu ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa Mhe Mizengo Peter Pinda nyumbani kwake eneo la Zuzu Jijini Dodoma.

Katika ziara hiyo Waziri Hasunga amempongeza Mzee Pinda kwa kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika sekta ya kilimo hususani katika kilimo cha mbogamboga na matunda kupitia kitalu nyumba (Green Houses) ambapo amesisitiza umuhimu wa uwekezaji huo kwa wakulima wa maeneo jirani kujifunza mbinu bora za kilimo kupitia yeye.

Pamoja na kutembelea ujenzi wa Vitalu nyumba kadhalika Waziri Hasunga amejionea uwekezaji mkubwa wa ufugaji wa kisasa wa samaki.

Akizungumza shambani hapo Waziri Mkuu mstaafu ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mhe Mizengo Peter Pinda amepongeza juhudi za Wizara ya Kilimo kuanzisha mchakato wa kuanzishwa kwa Sheria ya Kilimo itakayotoa suluhisho la changamoto zinazomkabili Mkulima na Sekta hiyo kwa ujumla itakayopelekea kuunganisha Bodi za mazao ili kuwa na mamlaka za mazao.

Kadhalika Mhe Pinda amesema kuwa kuna ulazima wa kuendelea kusimamia kwa weledi sekta ya Ushirika nchini kwani huo ndio umoja pekee unaowaunganisha wakulima na kuwa na nguvu ya pamoja hususani katika kupanga bei ya mazao yao kadhalika kuimarisha masoko ya mazao.

Kuhusu sekta ya Umwagiliaji Mhe Pinda amesema kuwa serikali inapaswa kuendelea kutilia mkazo zaidi kwani ndio njia pekee itakayomnusuru mkulima katika sekta hiyo ili kuondokana na kutegemea kilimo cha msimu wa mvua pekee.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...