Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
KLABU ya Yanga inatarajia kuchapisha nakala elfu hamsini (50,000) za jarida litakalozinduliwa alhamisi ya wiki hii.
Hayo yamesemwa na Afisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli wakati wa mahojiane yake na Kituo cha Redio cha EFM leo Jijini Dar es Salaam.
Bumbuli amesema wainatarajia kuzindua jarida hilo siku ya Alhamisi hii na litasambazwa nchi nzima.
Amesema, tayari wapo kwenye za mwisho na wanatarajia kuchapa nakala 50,000 za jarida hilo na litakuwa na makala na habari za ndani ya Yanga.
Bumbuli ameeleza kuwa, jarida hilo pia litakuwa na taarifa za kutosha kwa ajili ya wapenzi wa Soka kwa ujumla.
Mbali na hilo, Bumbuli amesema kutakuwa na gazeti la Wiki litakalokuwa na habari mbalimbali pia rasmi watazindua App ya Yanga itakayopatikana kwenye simu zote.
Kuzinduliwa kwa jarida hili linakuwa ni mara ya pili baada ya aliyewahi kuwa Afisa habari wa Klabu hiyo Dismas Ten kuchapisha jarida na kufanya vizuri sokoni na wadau mbalimbali kusifia kwa hatua kuwa klabu ya Yanga walichofanya ila sintofahamu baina ya viongozi ilisababisha kutokuchapishwa tena.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...