Na Emmanuel J. Shilatu
Ni
gumzo gumzo gumzo kila kona. Si vijiweni, sokoni, maofisini,
barabarani, majumbani, ama mitandaoni. Kote ni gumzo kufuatia hotuba
aliyoitoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe
Magufuli wakati akimuapisha Dk. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri mpya wa
Katiba na Sheria.
Awali
ya yote napenda kuungana na Mamilioni ya Watanzania kumpongeza Rais
Magufuli kwa hotuba hiyo murua aliyoitoa iliyoibua gumzo kubwa ndani na
nje ya nchi.
Watanzania
walijawa na hofu kubwa wanapoona zimepostiwa picha za Watu wamefariki,
wengine wakizikwa kutoka mitandaoni; mara wajuzi wakitueleza kila kifo
ni Corona. Wanakuja kuamini ya mitandaoni kufuatia taarifa ya Kiserikali
inayotoka kuonyesha idadi ya Wagonjwa ikiongezeka. Kumbe ongezeko lote
hilo inawezekana ndani yake kuna walioongezwa tu kutokana na kutokuwepo
kwa vipimo thabiti. Lakini Jana Rais Magufuli ulitutuliza mioyo yetu na
kuanza kuamini tatizo sio kubwa na kuanza kupuuza habari za mitandaoni.
Hata
WHO kupitia Mkurugenzi wake Mkuu Ndg. Tredos Ghebreyesu walikiri
vipimo vya wagonjwa wa COVID19 Afrika sio sahihi sababu ya vipimo sio
thabiti! Asante Rais wa JMT Baba John Pombe Magufuli kwa kutuweka wazi
juu ya hili. Hakika wewe ni Simba wa Afrika.
Ukazidi
kuwaondoa hofu mpaka Watumishi wa Umma juu ya hatma ya uchumi wao ambao
wengi walianza kuhisi waendapo hata mishahara watakosa lakini Jana
uliwapa uhakika kuwa utaendelea kuwalipa mishahara mpaka na Waalimu wote
ambao kwa sasa wapo likizo.
Katika
kuonyesha unasema kweli hata mshahara wa mwezi wa nne ulioisha
uliwalipa mapema sana Watumishi wa Serikali hata wale waliopo likizo.
Nchi nyingi zimeshindwa hili, lakini JPM Mwamba wa Afrika ameliweza
hili. Nani kama JPM?
Ahsante
sana Rais Magufuli kwa kutuondolea hofu, kutujaza matumaini mapya ya
kiafya na ya kiuchumi. Tunakuwahidi kuwa nawe bega kwa bega nyakati
zote tukishikamana nawe katika kupambana na adui Covid 19
anayesababishwa na kirusi Corona. Tupo pamoja sana Baba yetu Dk.
Magufuli.
Tanzania bila Corona inawezekana.
Jilinde; Nilinde; Tulindane
Wabheja sana!!
*Shilatu E.J*
0767488622
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...