Na Karama Kenyunko, Michuzi TV

Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu uchumi, imemuhukumu  Islem Shebe Islem  (50) raia wa Tanzania mwenye asili ya kiarabu, kutumikia kifungo cha miaka 30 gerezani baada ya kupatikana na hatia katika kosa la kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroine zenye uzito wa gramu 306.32.

Hukumu hiyo imesomwa leo Mei 8 2020 mbele Jaji Elinaza Luvanda baada upande wa mashtaka kupitia mashahidi wake saba na vielelezo mbali mbali zikiwemo dawa hizo kuweza kuthibitisha pasipo kuacha mashaka kuwa mshtakiwa ni mfanyabiashara wa dawa za kulevya.

Pia  mahakama imeamuru dawa hizo ziteketezwe  kwa mujibu wa sheria.

Akisoma hukumu hiyo, Jaji Luvanda amesema, amepitia kwa makini ushahidi wa upande wa mashtaka na utetezi uliotolewa na mshtakiwa mwenyewe pamoja na mashahidi wake wawili akiwemo dada yake Mariam Shebe na ameona kuwa mshtakiwa ana hatia hivyo anamuhukumu kifungo cha miaka 30 jela.

Awali kabla ya kusomwa kwa adhabu hiyo ya Jaji Luvanda aliuza upande wa mashtaka kama walikuwa na lolote la kusema ndipo wakili wa serikali Mwandamizi Mwahija Ahmed aliomba mahakama itoe adhabu kali mujibu wa sheria.

Naye mshtakiwa katika utetezi wake kupitia wakili wake Nehemia Nkoko ameiomba mahakama kumuhurumia mteja wake kwani ni mkosaji wa mara ya kwanza.

Islem ambaye alikuwa akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 11 ya mwaka 2019 alikamatwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Julai 20,2018 huko Magomeni ndani ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Sala

Mshtakiwa ametiwa hatiani kwa kukiuka Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya Namba 5 ya mwaka 2015 kama ilivyorekebishwa na Sheria Namba 15 ya  mwaka 2017.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...