Na.Vero Ignatus Arusha.

Jeshi la Polisi la Mkoa wa Arusha linamshikilia Daniel Emmanuel (32) Mkazi wa Sakila wilayani Arumeru,  kwa kukutwa akinywa damu ya mama yake Mzazi Eliyamulika Emmanuel Sarakikiya (79) kwenye kikombe, baada ya kumuua kwa shoka na kutenganisha shingo,mkono na mguu na kiwiliwili.

Akizungumza kwa masikitiko, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Jonathan Shana amesema mtuhumiwa huyo alifanya mauaji hayo Mei 15 mwaka huu, majira ya saa 9:00 mchana katika Kijiji cha Sakila chini,Kata ya Kikatiti,Tarafa ya King'ori wilayani Arumeru.

Mtuhumiwa huyo alimkata kwa shoka shingoni mama yake na kutenganisha na mwili wale na akaona haitoshi akakata mguu wa kulia na kuutenganisha na akakata mguu wa kushoto  pia akautenganisha wakati anafanya unyama huu alikuwa anakinga damu kwenye kikombe anakunywa,"alisema Kmanda Shanna

Amesema wakati alifanya tukio hilo majirani walishuhudia akinywa damu hiyo baada ya kumuua.

Kamanda Shana amesema hata hivyo polisi walipofika eneo la tukio mtuhumiwa alitupa kikombe alichokuwa ameshika mkononi kikiwa kimetapaa damu na kujaribu kukimbia.

"Lakini tulifanikiwa kumkamata na tumemweka mahabusu hadi upelelezi utakapokamilika,"amesema
Amesema katika hatua za awali za uchunguzi  inadaiwa mtuhumiwa huyo anamatatizo ya akili.

"Lakini hili sikubaliani sana sababu aliwezaje kuandaa shoka,mazingira tulivu yasio na watu,pia kwanini kama hana akili alikimbia polisi alipowaona na alipokamatwa alikataa kuhojiwa na polisi, hili linanipa shaka,"amesema


Amesema kutokana na hilo amemuagiza askari wa upelelezi wa kesi hiyo kuwasiliana na madaktari ili kumpima kama madai ya matatizo ya akili yana ukweli.

Ametoa wito kwa wananchi kupeleka ndugu zao  wenye matatizo ya akili polisi au hospitalini ili kuepuka madhara kama hayo.

Kamanda wa Polisi  mkoa wa Arusha Jonathan Shanna akionyesha waandishi wa habari shoka alilolitumia kijana huyo kufanyia mauaji ya mama yake mzazi na kikombe alichoweka damu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...