MSANII Mkongwe katika industry ya muziki, "AY" anayetamba na kibao cha Danhela ala shavu la Ubalozi wa simu mpya ya Infinix NOTE 7.
Kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii, @infinixmobiletz waliweka viashiria vya ubalozi huo wiki iliyopita na siku ya Jumamosi, Mei 9 walithibitisha ubalozi huo kupitia LIVE Session ya Instagram iliyo onyesha wawakilishi wa Infinix wakifanya mazungumzo na AY kuhusiana na simu ya Infinix NOTE 7.
Infinix NOTE 7 imepewa jina la Bigi Makini, na ndio sababu kuu iliyopelekea Infinix kufanya kazi na AY, kwani wengi tunafahamu AY ni msanii mkongwe mwenye mafanikio makubwa mwenye kuheshimika kutokana na mchango wake katika game la muziki Tanzania.
Ili kufahamu mengi zaidi kuhusiana na Infinix NOTE 7 na bidhaa nyengine za Infinix tafadhali tembelea kurasa zao za mitandao ya kijamii @infinixmobiletz
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...