Na Zainab Nyamka,Michuzi TV

ZIKIWA zimetimia Siku 66 toka kusimamishwa kwa Michezo mbalimbali ikiwemo soka sasa inatarajiwa kuanza mapema Mwezi Juni wadau wameendelea kujiuliza je Viwango vya wachezaji vitarejea kama awali.

Ikumbukwe kuwa Shughuli zote za kijamii ikiwemo mikusanyiko ilisimamishwa  na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa kutokana na janga la Virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19.

Kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoa maelekezo ya Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kutoa maelekezo ya michezo yote kurejea kama kawaida ifikapo Juni 01.

Wadau mbalimbali wa michezo wamepokea kwa furaha kubwa hatua hiyo baada ya kukaa muda mrefu bila kupata burudani pendwa ikiwemo mchezo wa Soka.

Je, kurejea kwa Ligi hiyo wachezaji watarudi wakiwa na viwango vyao vya awali au watahitaji muda zaidi kujiandaa??

Hilo ni swali ambalo wadau wote wa soka wamekuwa wanajiuliza kama wachezaji wameweza kujilinda katika kipindi chote hiki na kufuata maelekezo (programu) ya mwalimu ili kulinda viwango vyao visishuke.

Kila Kocha alitoa programu kwa wachezaji wake katika kipindi chote pamoja na maelekezo  mengine wayafuate katika kipindi hiki ambapo Ligi hazichezwi.

Makocha waliona kuna umuhimu wa kuwapa wachezaji programu maalumu ili wajiweke tayari kwa muda wowote pale Ligi itakapoamuriwa ianze, nalo ni jambo jema.

Katika pita pita zangu, katika Viwanja vya mchangani, fukwe za bahari na hata kwenye mitandao ya Kijamii nimeshuhudia wachezaji wakifanya mazoezi binafsi iwe asubuhi au jioni na wengine wakijumuika wakiwa wawili au watatu ili mradi watimize majukumu waliyoachiwa.

Hili sio baya, lakini swali langu linabaki Ligi itaanza ndani ya muda mfupi timu itahitaji mazoezi ya pamoja angalau wiki 2 au siku 10 ili waweze kurejesha utimamu wa mwili  kabla ya kuanza kucheza mechi za ushindani.

Wachezaji watahitaji mechi za kirafiki, kupata fikizia  lakini je kwa muda uliopo wataweza? Jibu ni hapana

Kurudi kwa viwango vya wachezaji ni suala la mchezaji husika kufuata programu ya mazoezi  aliyopatiwa na mwalimu, kujitunza ikiwemo kupata muda wa kupumzika na kula vizuri.

Iwapo wachezaji watakuwa wamefuata taratibu zote la hasha itawachukua mechi mbili hadi tatu kukaa sawa katika utimamu wa mwili na kurejea kwenye viwango vyao vya kawaida.

Shirikisho la Soka Duniani FIFA waliweza kufikiria suala la wachezaji kukaa muda mrefu kuwa na mechi na kuona kuna umuhimu wa kubadili sheria namba 3 katika kipengele cha Mabadiliko ya wachezaji wa akiba kutoka watatu hadi watano.

Hii ina maana kuwa kwa FIFA wamechukulia uzito wa suala la afya za wachezaji kwa kuongeza idadi ya wachezaji wa akiba kitoka watatu hadi watano katika mchezo mmoja.

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe ametoa maagizo kwa klabu zote kuanza kujiandaa na muendelezo wa Ligi Kuu utakaoendelea kuanzia hivi karibuni na kuchezwa kwenye Viwanja Vitatu Uhuru, Uwanja ww Taifa na Chamazi Complex.

Na Ligi daraja la kwanza na La Pili kuchezwa Jijini Mwanza wakitumia uwanja ww CCM Kirumba na Nyamagana.

Sasa kilchobaki ni benchi la ufundi kuanza mchakato wa kuandaa pramu kwa ajili ya wachezaji pindi wanaporejea kwa ajili ya mazoezi ya pamoja kujiandaa na Ligi.

Je kwa wale wachezaji walioko nje ya nchi, makocha walioko kwenye nchi zao wataweza kurejea na kuendelea na Ligi au itawalazimu kusubiri kwanza??

Tukutane tena Kwa Mkapa, Uhuru na Chamazi, Watu tulilimisi soka bhana.....
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...