Pichani anaonekana Fundi Bomba kutoka BUWASA Ndg. Vicent Mashauri akimuelekeza mtoto namna ya kunawa Mikono katika zile hatua zinazoelekezwa na Mamlaka za Afya.
 Pichani ni Mkuu wa Wilaya za Bukoba Mhe. Deodatus Kinawiro akizindua kwa Vitendo Vizimba Vitatu vilivyojengwa na BUWASA lengo likiwa ni Wananchi na Jamii kwa ujumla waendelee kunawa mikono kama tahadhari ya Corona.
 Pichani. Ndoo zipatazo Thelathini zilizotolewa na BUWASA tayari kugawiwa katika maeneo mbalimbali hasa vituo vya Afya kabla ya kukabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya Bukoba.
 Pichani anaonekana Mwenyekiti wa Bodi ya BUWASA Ndg. Samora akikabidhi Ndoo Thelathini kwa Mkuu wa Wilaya za Bukoba Deodatus Kinawiro katika tukio lililofanyika eneo la Soko kuu Bukoba.
 Pichani anaonekana Mama akianawa Mikono katika kizimba kilichopo eneo la Stendi kuu ya Mabasi Bukoba kama alivyokutwa na kamera yetu.
 Pichani Muonekano wa Ndoo mojawapo kati ya Ndoo Thelathini zilizotolewa na BUWASA ikiwa kila moja ina thamani ya Shilingi elfu kumi na Saba.


Na Abdullatif Yunus - Michuzi TV

Mapambano dhidi ya Virusi Vinavyoeneza homa kali ya Mapafu Corona yanaendelea kuchukua sura mpya ndani ya Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera, wakati ambapo Jamii inashauriwa kuendelea kuchukua tahadhari juu ya Ugonjwa huu unaosababishwa na Virusi aina ya Covid-19.

Katika kuzingatia hayo Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bukoba (BUWASA) Wameamua kuendeleza mapambano hayo kwa kujenga vizimba vitatu vya kunawia mikono pamoja na kutoa Ndoo thelathini za kunawia mikono ndani ya Manispaa ya Bukoba, vyenye jumla ya thamani ya zaidi ya  Shilingi Milioni Nne, ikiwa pia ni sehemu ya kurudisha fadhila kwa wateja wao.

Awali kabla ya kukabidhi Vifaa hivyo na miradi hiyo Mkurugenzi wa BUWASA Ndg. John Sirati ameeleza ndani ya Taarifa fupi ya miradi hiyo kuwa, Mamlaka imeamua kuweka huduma hiyo ya Maji bila tozo katika Stendi ya dharula ya Mabasi madogo, Stendi Kuu na Soko kuu la Bukoba, na kwamba hakutakuwa na malipo ya Ankara ya Maji kwa kipindi chote cha mlipuko wa ugonjwa huu wa Corona.

Akipokea Vifaa hivyo Mkuu wa Wilaya Bukoba, Mhe. Deodatus Kinawiro na kisha kuukabidhi kwa Mkurugenzi wa Manispaa amewataka Viongozi wa Soko na wananchi kutumia Vifaa na miradi hiyo kwa uangalifu na malengo yaliyokusudiwa hasa kulingana na teknolojia inayotumika.

BUWASA Pamoja na mambo mengine tayari imeendelea kuhakikisha huduma ya Maji inapatikana wakati wote hasa kipindi hiki cha Corona, na kwamba itarejesha huduma ya maji kwa wateja waliositishiwa bila faini, sambamba na hilo tayari mamlaka imeandaa gari la Maji safi kwa ajili ya kupeleka Maji sehemu yoyote ambayo itakayoonekana ina dharula au uhaba wa Maji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...