Imeelezwa
kuwa changamoto ya utoaji wa fedha za fidia kwa nchi zenye kuleta
athari ya mabadiliko ya Tabianchi duniani kwa kiwango kikubwa imekuwa ni
Tatizo hivyo inahitajika mjadala mpana kuokoa hali ya athari za
mabadiliko ya Tabianchi kwa nchi changa duniani.
Hayo
yamebainishwa kwenye mjadala wa kamati ya Kilimo Maliasili na Utalii ya
bunge la Afrika mashariki na mbunge wa bunge hilo Josephine Lemoyan
wakati alipokuwa akiongea na vyombo vya habari Mara baada ya kikao Chao
kwa njia ya Mtandao mapema Jana kwenye makao makuu ya Jumuiya hiyo
jijini Arusha.
Alisema
kuwa mjadala huo unahitajika Sana kuweza kusaidia kuongeza mapambano
hayo kwani kumekuwa na nchi ambazo zimeshindwa kuhoji suala hilo la
kupata fedha za kupambana na athari za mabadiliko ya Tabianchi duniani
kwa Sasa.
"Tunawezaje
kuwalazimisha wanaotoa fedha kutoa kwa wakati kama walivyoahidi kwenye
mikataba ya kupambana na athari ya uharibifu wa Tabianchi kote duniani
pasi na kuwa na mjadala wa kina wa kuzungumzia suala hilo ili kufikia
muafaka wa mikataba hiyo"
"Tunapozungumzia
mabadiliko ya Tabianchi sio kwa kipindi kimoja tunahitajika
tuyazungumze kwa kina kila Mara kwani kumekuwa na athari kwa nchi zetu
huku fedha na vifaa ikiwa ni changamoto kubwa kwa nchi zetu" alisema
Lemoyan
Alisema kuwa
masuala ya mazingira hayahitaji subra kuyazungumza kwa yamekuwa yakileta
athari mbalimbali miongoni mwa jamii zetu ikiwemo majanga ya mafuriko
ifike mahali tuwe na Kitengo Cha maafa kwa nchi zetu za Eac.
Akabainisha
kuwa nchi zetu kiwango Cha uharibifu wa mazingira ni asilimia 25 na
tunahitaji kuwa na usalama wa chakula huku mabadiliko ya Tabianchi
yakiendelea kutuathiri utaona jinsi hivyo tukiwa na mfuko wa pamoja wa
majanga utasaidia kuomba fedha pamoja na kujichanga ili kukabiliana na
suala hilo la usalama wa chakula kwa nchi zetu.
"Uwepo
wa mikakati mbalimbali ya pamoja wa kuweka viashiria vya majanga kwa
pamoja kwani Utakuta Janga linaanzia nchini Kenya linaishia Rombo nchini
Tanzania ifike mahali tukazungumza kwa Umoja wetu jinsi ya kuangalia
namna nzuri ya kukabiliana na athari hizo"
Wakichangia
mjadala huo wabunge kutoka nchini Burundi walienda mbali na kutaka
kuundwa kwa mfuko wa pamoja kwa nchi za Jumuiya hiyo ili kukabiliana na
athari za mabadiliko ya Tabianchi kwenye Ukanda huo.
Walisema
mfano nchi hiyo imekuwa na muingiliano ya kimipaka mfano Ziwa
Tanganyika hivyo kutaka Juhudi za pamoja za kupambana na athari za
mabadiliko hayo kwa umoja wao.
Walibainisha
kuwa miradi mingi ya Utekelezaji wa athari za mabadiliko ya Tabianchi
fedha zake zinatoka kwenye nchi zenye kuharibu mazingira kwa kiwango
kikubwa hususani nchi za magharibi hivyo mpango wa pamoja ikiwemo
mijadala kwenye mikutano yao inahitaji kwa kipindi hiki.
Burundi
imeridhia itifaki ya mikataba sita ya masuala ya athari za mabadiliko
ya Tabianchi na haipo nyuma Sana kwenye utekelezaji wake imeonyesha
jinsi athari hizo kwenye sekta ya Kilimo Rasilimali za maji huku
ikizitaka nchi za Eac kuhamasisha wananchi kupanda mbegu zenye kuhimili
mvua kidogo kutokana na athari hizo za Tabianchi.
Nao
wajumbe kutoka Sudani kusini ambao nchi yao bado ni mwanacha mchanga
ambaye bado mifumo ya kitaasisi ni changamoto ikiwemo bajeti na
wataalamu kwa kuwa inajenga nchi yao Ila sera na mifumo inangojea
kupitishwa na Serikali siku zijazo huku ikiridhia itifaki hizo.
Walisema
kuwa wamekuwa wakishirikiana na mashirika ya kimataifa katika kuona
wanakabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwani wamekuwa na changamoto ya
vifaa vya kupima hali ya hewa kutokana na uchanga wa nchi yao.
Walieleza
kuwa wananchi bado hawajahusishwa kwenye masuala ya kiuchumi ambayo
yanaleta mabadiliko ya Tabianchi huku udhibiti wa makampuni ya mafuta na
madini ndani ya nchi hiyo ukiwa bado ni changamoto ya uharibifu wa
mabadiliko ya Tabianchi
Wajumbe
kutoka Rwanda walisema kuwa nchi hiyo inazo Taasisi zinazojihusisha na
udhibiti wa masuala ya mabadiliko ya Tabianchi lakini changamoto yao ni
kilimo Cha kienyeji ambacho limekuwa kikileta athari za mabadiliko ya
Tabianchi.
Pia wamekuwa
na tatizo la uwekezaji katika Kitengo Cha udhibiti wa masuala ya
Tabianchi,ikiwemo ukosefu wa fedha za ndani kukabiliana kwa kuwa nchi
hiyo Ina milima na mabonde hali inayotatiza nchi hiyo katika kukabiliana
na athari za mabadiliko ya Tabianchi.
Mjadala
huo ulioendeshwa kwa njia ya Tehama kwa wajumbe wa nchi Tatu za
Rwanda,Burundi na Sudani ya Kusini kueleza jinsi athari za mabadiliko ya
Tabianchi kwenye nchi zao unatarajiwa kuendelea kwa nchi za
Tanzania,Kenya na Uganda kueleza changamoto na mafanikio kwa nchi zao
kwenye kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabianchi na mikakati yao
siku ya kesho.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...