RUZUKU ya dola za kimarekani milioni  (UDS) 4.75 kusimamiwa na  Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia ya Tanzania (COSTECH) ili kufanikisha Uchunguzi, Kinga na Tiba ya ugonjwa wa Corona (COVID-19).

Hayo yamesemw na Mkurugenzi Mkuu wa  Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia ya Tanzania (COSTECH), Dk.Amos Nungu wakati akizungumza na waandishi wa habari kupitia mtandao wa video leo. Amesema kuwa uratibu wa fedha hizo ni sehemu ya majukumu ya Tume  hiyo ikiwa ni pamoja na  kutafuta rasilimali fedha (resource mobilization) ili kuendeleza utafiti. 


Amesema kuwa Jumla ya fedha iliyotolewa kwa sasa ni dola za kimarekani milioni 4.75 (USD) zilizotolewa na wadau mbalimbali wa maendeleo kupitia Taasisi ya Taifa ya Utafiti ya Afrika Kusini (NRF). 

"Ruzuku hii inahusu nchi 15 zilizo ndani ya 'Science Granting Councils Initiative' ambazo ni (Botswana, Burkina Faso, Côte d’Ivoire, Ethiopia, Ghana, Kenya, Malawi, Namibia, Mozambique, Rwanda, Senegal, Tanzania, Uganda, Zambia, na Zimbabwe). 

Dk. Nungu amesema kuwa lengo la ruzuku ni kufanikisha upatikanaji wa maarifa kuhusiana na huu ugonjwa  wa Corona (COVID-19) ili kufanikisha Uchunguzi, Kinga na Tiba.

"Maeneo matatu yatakayofadhiliwa ni 1. Research, 2. Science engagement – Waandishi habari, washauri." Amesema Dk. Nungu

Amesema kuwa Wadau wa maendeleo waliochangia katika hii ruzuku ni pamoja na  Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo la Kimataifa la Sweden (Sida), Kituo cha Utafiti cha Maendeleo cha Kimataifa cha Canada (IDRC), Idara ya Uingereza ya Maendeleo ya Kimataifa (DFID). 

Dk.Amos M. Nungu anatoa rai kwa wadau wote waliolengwa kuanza maandalizi ya kuleta maandiko yatakayo stahimili ushindani na maelekezo ya kina na fomu za maombi zinapatikana https://www.nrf.ac.za/division/funding/covid-19-africa-rapid-grant-fund

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...