Mzee Salvatory Magayana akimuelekeza mjuukuu  wake (mwenyekofia) nanna ya kuunganisha mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu za sumaku.
Mwalimu wa Ufundi chuo cha Ufundi VETA Mwanza, Lawrence Mashindano (wa kwanza kushoto) akimwelekeza Mzee Salvatory Magayana namna yakutumia mashine za kisasa katika kuboresha mtambo wake wa kuzalisha umeme wa nguvu za sumaku.

TUME ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) yamwezesha Mbunifu mwenye umri wa miaka 80 katika kutengeneza nishati ya umeme kwa kutumia sumaku.


Katika kuelekea uchumi wa viwanda nchi inahitaji umeme mwingi, wa uhakika, gharama nafuu na unaotabirika. Taifa lolote linalotamani kuwa na maendeleo endelevu, ni lazima lihakikishe nishati ya umeme inapatikana kwa uhakika kwani ndiyo mhimili muhimu wa maendeleo na ukuaji wa uchumi.
 
Ni kwa kutambua hilo, Serikali ya Awamu ya Tano imejikita zaidi kuwekeza kwenye miradi ya kimkakati ya kufua na kusambaza huduma ya umeme kote nchini Tanzania.
kwa sasa nchini kuna  umeme wa kutosha ambapo kuna megawati takriban 1600 na umeme unao tumika ni megawati 1092 lakini bado hauwezi kutosheleza mahitaji ya miaka ijayo kwenye kujenga uchumi wa viwanda.

Hivyo Tanesco  inatakiwa kuzalisha umeme wa kutosha, wa uhakika na unaotabirika lakini pia wa bei nafuu na hivyo utekelezaji wa mradi mbalimbali  ni muhimu sana.

Wastani wa asilimia 50 ya megawati zinazozalishwa zinatokana na umeme unaozalishwa kwa gesi na kuongeza kuwa uchumi wa viwanda unahitaji umeme wa uhakika unaotegemea vyanzo mbalimbali vya uzalishaji umeme.

Aidha, Serikal ilisema  itaendelea kuzalisha umeme kupitia vyanzo tofauti ikiwemo makaa ya mawe, gesi, joto radhi, upepo na mingine mingi kupitia Waziri wa Nishati Dkt Merdard Kalemani  Mkoani Njombe katika kikao kilichoshirikisha wadau mbalimbali wa ujenzi Miradi wa Maporomoko ya maji mto Rufiji (Rufiji Hydropower Project).
.
  Mzee Salvatory Magayana akiongea na waandishi wa habari namna alvyoanza ubunifu wake wa  kuzalisha umeme wa nguvu za sumaku.

Chanzo kikubwa cha maji katika mradi wa Maporomoko ya mto Rufiji ni Mto Kilombero, Ruaha Mkuu na Mto Wegwe.

Mito hiyo inapata maji kutoka vyanzo vya maji vya nyanda za juu kusini hususani maeneo ya Njombe, Makete na Waging'ombe.

JUHUDI ZA SERIKALI KUZALISHA UMEME
Serikali inatambua mchango wa waendelezaji wa nishati ambao hadi sasa wamezalisha umeme wa takribani 17MW ambao umeingizwa katika gridi ya Taifa na mwingine kuwauzia moja kwa moja wananchi wa vijijini.

Waziri Kalemani anasema kuwa kuna  dola za Marekani Milioni 54.5 kwa ajili ya kuwawezesha wawekezaji binafsi.

Fedha hizi zimetengwa kwa Mwaka wa Fedha 2019/20. Aidha Dr. Kalemani alisisitiza kuwa, Serikali imeweka lengo la kuzalisha umeme wa 10,000MW ifikapo Mwaka 2025, hivyo anategemea waendelezaji binafsi wachangie katika uzalishaji huu ili kufikia lengo hilo.

Alisema kuwa waendelezaji miradi wote walioingia mikataba na REA ya kusambaza umeme katika vijiji 120, hadi sasa ni vijiji 82 kati ya hivyo vimefikiwa na huduma ya umeme na kuagiza vijiji vilivyobaki vikamilishwe ili kutimiza Mpango wa Serikali wa Kusambaza Umeme Vijijini (2016/17 – 2021) la kufikisha huduma ya umeme katika vijiji vyote ifikapo Juni 2021.

MCHANGO WA COSTECH KATIKA KUPATIKANA UMEME
Ili kuchangia juhudi za Serikali katika kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na nishati ya umeme wa kutosha, Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imemwibua na kumuwezesha Mbunifu mzee Salvatory Magayana mwenye umri wa miaka 80.

Mzee Magayana amebuni njia ya kuzalisha nishati ya umeme kwa kutumia sumaku.

Mzee huyo ni miongoni mwa wabunifu kutoka sekta isiyo rasmi ambaye kutokana na uzoefu wake wa miaka mingi wa ufundi wa umeme kwenye magari na pikipiki, amebuni mfumo unaozalisha nishati hiyo kwa kutumia sumaku.

Ubunifu wa kuzalisha nishati ya umeme kwa kutumia sumaku ulimfanya Mzee Magayana awe miongoni mwa zaidi ya wabunifu 50 walionufaika na ruzuku ya Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Tekonolojia na Ubunifu (MAKISATU) unaoratibiwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa ajili ya kuwaibua wabunifu na kuishauri Serikali namna ya kuwaendeleza wabunifu hao.

COSTECH teyari imemsadia Mzee Magayane kwa kumwendeleza ubunifu wake kwani kwa sasa anahudhuria mafunzo ya ufundi katika chuo cha ufundi VETA tawi la Mwanza.

Kitendo cha kuanza mafunzo ya kujengewa uwezo katika ubunifu wake kilimfurahisha sana mzee Magayana na anasema “Nilikuwa najua VETA ni kwa ajili ya vijana wadogo. Yaani siamini kama nipo hapa. Nafurahia mafunzo yanayotolewa na wataalamu, kwa kweli yanarahisisha sana ubunifu wangu”.

Mzee huyo mkazi wa Kijiji cha Namibu wilayani Bunda anasema mtambo aliobuni unaotumia sumaku unaweza kuzalisha nishati ya umeme unaotosha kuendeshea shughuli mbali mbali za kiuchumi.

Ubunifu huo unalengo la kuwasaidia hasa wananchi wa kipato cha chini kama vile wavuvi wanaotumia boti ya injini, wamwagiliaji wanaovuta maji kwa jenereta au mashine za kukoboa na kusaga maeneo ya vijijini zinazotumia nishati ya mafuta ya petroli au dizeli.

Pia Mzee Magayana amelenga kutatua changaoto wa watu wanaotumia nishati ya mwanga wa jua kuzalisha umeme kwani wakati wa masika huwa kuna changamoto ya upatikanaji wa nishati hiyo sababu ya mawingu yanapotanda muda mrefu.

“Kuna gharama kubwa kutumia mashine zinazo endeshwa kwa mafuta. Kununua mafuta ni gharama kubwa nataka kutatua changamoto hiyo. Mtu awe anamwagilia shamba lake bila gharama hizi. Hata wavuvi au wanaosaga nafaka, wawe na uhakika wa shughuli zao bila hofu ya umeme au mafuta,” anasema mbunifu huyo.

Mwaka 2018/19 Mheshimiwa Waziri Ndalichako alisema kulikuwa na wabunifu 415 walijitokeza kushiriki MAKISATU na baada ya mchujo wakabaki 60 yaani 10 kutoka katika kila kundi la sekta isiyo rasmi, vyuo vikuu na makundi mengine.

“Wabunifu watatu mahiri kwa kila kundi walipatikana na kupewa tuzo na Ubunifu wao utaendelezwa. Serikali imekusanya taarifa na kutambua teknolojia 165 zilizozalishwa nchini kwa lengo la kupata takwimu zitakazotumika kutengeneza kanzidata ya teknolojia zinazoweza kutumika kutatua changamoto zilizopo na kuchangia uchumi wa viwanda nchini,” alisema mheshimiwa Waziri Ndalichako.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...