Na Amiri kilagalila,Njombe

Serikali wilayani Njombe imeagiza wafanyabishara wa Sukari wilayani humo kuzingatia bei elekezi iliyopangwa na serikali kufuatwa katika mkoa huo ili kudhibidi mlipuko na wizi unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara.

Ili kudhibiti kasi ya ongezeko la bei ya sukari nchini serikali imepanga bei ya sukari kwa kila mkoa kulingana na mazingira na mahitaji kwa kuzingatia sherikali sheria ya Sukari No 26 ya Mwaka 2001(Cap. 251) chini ya kifungu cha 11A ambayo imeutaka mkoa huo kuuza sukari kwa bei ya jumla mfuko wa kg 50 jumla kwa shilingi 135000 ambapo kg 1 itauzwa shilingi 2700 huku bei ya reja reja ikiagiza kuuzwa shilingi 2900

Akitoa agizo hilo alipokutana na wafanyabiashara wa sukari mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri anasema wafanyabiashara wamekuwa wakijipangia bei kwa matakwa yao jambo ambalo linawaumiza wananchi na kwamba kuanzia sasa watapaswa kuzingatia bei elekezi bila kujali mazingira ya upatikanaji wake.

Aidha Dc Msafiri amesema ili kuhakikisha takwa hilo la kisheria linatekelezwa ni muda wowote timu ya ulinzi na usalama itaingia mtaani kufanya ukaguzi kama bei hizo zinafuatwa.

“Na kamati yangu ya usalama,itanisaidia kuhakikisha kwamba bei hizi tulizoletewa kuhakikisha tunazitekeleza kuanzia sasa”alisema Ruth Msafiri

Baadhi ya wafanyabiashara ambao wameshiriki katika kikao hicho akiwemo Rodrick Sanga na Harid Mbilinyi wanasema wamepokea agizo hilo lakini wanaiomba serikali kuwasaidia kupata sukari kwa kuwa mkoa huo umeishiwa kabisa sukari.

“Sukari mpaka tunavyoongea hivi Njombe hamna,na muuzaji Dar es Salaam ni mtu mmoja,sawa tumepokea hilo lakini sukari hatuna tunaomba tupate maelekezo labda tutaipata kwa nani” Alisema Rodrick Sanga

Katika hatua nyingine mkuu wa wilaya amepiga marufuku kwa wafanyabishara ambao watathubutu kuficha sukari ili waweze kuja kuuza baadae kwa faida zaidi na kwamba hadi sasa bei ya sukari imekuwa ikiuzwa zaidi ya elfu 3100.

“Serikali inajua njia zote inako tokea Sukari,lakini kinyume na bei hii mtu asinunue sukari,na sisi wakati wowote ule tutajipanga kuhakikisha tunakagua uwepo wa sukari”alisema Msafiri Wakati serikali ikipanga bei ya shilingi elfu 2900 ya sukari katika mkoa wa Njombe ,mkoa wa Iringa ni shilingi 2900, Mbeya 3000 huku Katavi na Ruvuma zikipewa shilingi 3200.
 Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...