KILOMBERO, MOROGORO.
KILA Binadamu anapitia mapito aliyoandikiwa na muumba wa Dunia. Kila pito lina njia yake ya kuingia na kutokea.
KILA Binadamu anapitia mapito aliyoandikiwa na muumba wa Dunia. Kila pito lina njia yake ya kuingia na kutokea.
Tunaamini mpendwa wetu Bwana. GEOFREY JULIUS MCHANGA (Pichani) yupo katika mapito, hakika kwa pamoja tukiungana tutaweza kumsaidia kuwa katika hali yake kama awali.
Kwa sasa msaada wa haraka unahitaji zaidi kuokoa maisha yake akitakiwa kwenda Dar es Salaam (Muhimbili).
Anatakiwa kufanyiwa vipimo zaidi na upasuaji wa matatizo yake yanayomkabili ya maradhi ya ukubwa wa Moyo, mapafu kuwa na ukungu na tezi shingoni (tezi ya shingo).
Matibabu hayo yanahitajika kufanyiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).
Gharama za awali za kuanzia matibabu yake ni shilingi Milioni moja na Laki tano (1,500000 ).
Na kiasi cha chini cha shilingi Laki tano kwa ajili ya gharama za matumizi ya usafiri, malazi na chakula yeye na msimamizi wake.
Hivyo tunakuja kwenu kuomba chochote ilikufanikisha kiasi cha shilingi Milioni 2.
Kwa sasa jukumu hilo linasimamiwa na vijana aliomaliza nao kidato cha nne 2013 wakiongozwa na Sweatbert P James ama MC Zakayo Mtozaushuru wa Mtozaushuru Entertainment.
"Sisi vijana kwa pamoja ambao tulisoma nae 2013 tunakuja mbele yako kuomba msaada wa hali na Mali kwa niaba ya ndugu yetu mpendwa, Bwana Geofrey.
Kwa mujibu wa Madaktari wa awali alipokuwa akipata tiba huku Kilombero wamependekeza apelekwe Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi ya kina." Alisema Sweatbert Jamese 'Lazaro Mtozaushuru'.
Kwa mawasiliano zaidi/kutuma msaada wako tumia namba ya MC ZAKAYO MTOZAUSHURU jina la usajili litatokea SWEATBERT P JAMES:
+255 688 523 165.
Namba ya Geoffrey (Muhitaji wa matibabu):
+255677671984.
AU;
Msaada wa kuweza kupata Daktari atakayesaidia kumpatia matibabu ya haraka.
"Lengo letu sote ni kuhakikisha ndugu yetu ana rejea katika hali yake ya kawaida. Yote yana wezekana kwa msaada wa Mwenyezi Mungu".
Hadi sasa Geoffrey ameshapata barua ya rufaa kupelekwa Muhimbili, lakini hatuna hata ya kuanzia.
"Tunamuangaikia fedha za chakula na mahitaji mengine hali yetu ni duni sana, hivyo tunazidi kuwaangukia Wadau, ndgu, marafiki na jamaa popote pale mlipo".
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...