Na Said Mwishehe, Michuzi TV.

ANAYEJUA Aanajua tu!Hivyo ndivyo unavyoweza kuzungumzia video mpya ya wimbo wa Quarantine ambayo imeachia siku tatu zilizopita na Msaani mwenye ubora wake katika muziki wa kizazi kipya Naseeb Abdull a.k.a Diamond akiwa amesherikiana na wasanii wenzake wa lebo ya WCB.

Ukweli kwa mara ya kwanza Diamond kupitia wimbo huo umemfanya kuwa gumzo kutokana na wasanii maarufu nchini Marekani kukubali video ya wimbo huo .Na sio tu kuikubali bali video ya wimbo huo inashika nafasi ya 39 katika video ambazo zinatamba nchini Marekani. Kwa kukumbusha tu kwa Tanzania video ya wimbo huo ndio inayoonngozwa kwa kutazamwa zaidi na kuifanya kushika namba moja kwenye mtandao wa You Tube.

Awali video hiyo ya Quarantine katika nchi hiyo ya Marekani ilikuwa inashika nafasi ya 40 lakini leo hii imepanda hadi nafasi ya 39, hali iliyomfanya Diamond kushindwa kuficha furaha aliyonayo moyoni mwake kwa kuendelea kufanya vizuri na kiwango kikubwa kama hicho ambacho hatimaye wanamuziki waMarekani wamekitambua.

Kupitia mtandao wake wa kijamii Diamond ameandika ujumbe mzito wa kutos shukrani zake kwa wanamuziki wa Marekani kwa kuikubali video ya wimbo wa Quarantine huku akieleza wazi hivi sasa ndio unaweza kujua aliposema Quarantine ndio nyimbo ya Dunia zima.Hivyo ameamua kusherehekea video hiyo kupasua anga la muziki kutoka kwenye ardhi ya JPM hadi kwa Donald Trump huko Marekani.

Hata hivyo wakati video hiyo ikishika nafasi ya 39 katika video ambazo zinatamba kwa sasa nchini Marekani, pia nchi nyingine mbalimbali duniani nazo zimepokea video hiyo kwa mikono mwili .Baadhi ya nchi hizo ni Canada ambapo video hiyo ya Quarantine inashika nafasi ya 37 kwa siku ya leo kutoka nafasi ya 26 wakati nchini Ufaransa imewezesha kushika nafasi ya 40 ingawa kwa sasa inashika nafasi ya 56.Katika nchi ya Kenya video ya wimbo huo inashika nafasi ya pili huku nafasi ya kwanza ya video ambayo imeshika namba moja nchini humo ni ya Sauti Solo Katika nchi ya Uganda video ya Quarantine imefanikiwa kushika nafasi ya nane.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...