Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe.Selemani Jafo akizindua Kituo cha Afya Sunya, kilichopo wilayani Kiteto Mkoani Manyara.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe.Selemani Jafo akipiga makofi baada ya kuzindua Kituo cha Afya Sunya, kilichopo wilayani Kiteto Mkoani Manyara.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe.Selemani Jafo akiongea na watumishi Kituo cha Afya Sunya, wakati wa uzinduzi wa kituo hicho  kilichopo wilayani Kiteto Mkoani Manyara.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe.Selemani Jafo akikagua vifaa vya vilivyopo katika Kituo cha Afya Sunya, kilichopo wilayani Kiteto Mkoani Manyara.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe.Selemani Jafo akizungumza na uongozi wa Halmashauri ya wilaya Kiteto leo katika ukaguzi wa jengo la utawala la halmashauri hiyo.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Selemani Jafo akikagua jengo la Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, Manyara alipofanya ziara ya kikazi wilayani humo leo.
 Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Manyara, Tumaini Magese akizungumza wakati wa Uzinduzi wa kituo cha afya cha Sunya wilayani hapo uliofanywa na Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo
 Muonekano wa Jengo la Ofisi ya Halmashauri ya Kiteto ambalo Waziri Jafo amelitembelea na kukagua Ujenzi wake leo.

 Muonekano wa juu wa kituo cha Afya cha Sunya kilichopo wilayani Kiteto, Manyara ambacho kimezinduliwa leo na Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo.

……………………………………………………………………

Charles James, Michuzi TV

SERIKALI imewataka wataalam wa Afya nchini kujipanga vema katika kutoa huduma bora kwa wananchi ili kutimiza lengo la Rais Dk John Magufuli la kuwatumikia watanzania

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Selemani Jafo leo wakati akizindua Kituo Cha Afya cha Sunya kilichopo wilayani Kiteto Mkoani Manyara.

Jafo amewataka wananchi kuhakikisha wanalinda miundombinu ya kituo hicho ili dhamira ya serikali ya kusogeza huduma za afya karibu na wananchi iweze kutimizwa .

Amesema kituo hicho kutakua msaada mkubwa kwa wananchi wa Wilaya hiyo na hivyo kutatua changamoto iliyokuepo ya kukukosekana kituo cha afya katika kata hiyo ya Sunya na hivyo kuwalazimu wakazi hao kufuata huduma za afya umbali mrefu.

" Ukosefu wa kituo cha afya katika kata hii kulilazimu wananchi kwenda wilayani Kilindi mkoani Tanga au kusafiri kilomita 125 kufuata huduma katika hospitali ya wilaya.

Niwaombe wananchi mshirikiane katika kutunza miundombinu ya kituo hiki,sitarajii nikija hapa nikute mmeharibu koki hapana,kila mtu awe mlinzi wa mwenzake ili kituo hiki kiwe na manufaa kwa sisi na vizazi vyetu vijavyo,” Amesema Jafo.

Jafo amesema kuwa  kituo hicho ni miongoni mwa vituo vilivyopewa kiasi cha shilingi milioni 400 na ujenzi umekamilika kwa kiwango alichoridhika nacho.

Katika hatua nyingine pia Jafo amekagua ujenzi wa jengo la halmashauri na kumtaka mkandarasi wa Pacha Construction LTD kukamilisha ujenzi kwa wakati uliyopangwa.

" Mkurugenzi ninachosisitiza hapa kazi ikamilike kwa wakati na niwaambie hili jengo likikamilika litakuwa ni miongoni mwa halmashauri zenye ofisi nzuri nchini,lakini wakati mwingine jitahidi gharama ziwe ndogo tofauti na hizi za sasa hivi,” Amesema  Jafo.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya hiyo, Tumaini Magese ameiomba serikali kuwaongezea vituo vya afya viwili ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya kutokana na ukubwa wa wilaya hiyo.

Akitoa taarifa ya ujenzi huo Mkurugenzi wa halmashauri ya Kiteto, Tamimu Kambona amesema kuwa ujenzi huo ulianza januari 2018 na umekamilika mwaka 2019 kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 510 na wananchi elfu 38,273 wanatarajiwa kupata huduma katika kituo hicho.

Kambona amesema kuwa fedha zilizotumika ni shilingi milioni 483.4 na kiasi cha milioni 35 ni bakaa ambazo zitatumika kwa ajili ya kujenga duka la dawa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...