JUNI 15, 2020 MWISHO USAJILI WA MIRADI YA
UCHENJUAJI DHAHABU (LEACHING AND ELUTION PLANTS) KWA AJILI YA TATHMINI YA
ATHARI KWA MAZINGIRA (ENVIRONMENTAL IMPACT ASSESSMENT) NA UKAGUZI WA MAZINGIRA (ENVIRONMENTAL
AUDIT)
Baraza
la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) linawatangazia wawekezaji
wote wanaojihusisha na shughuli za uchenjuaji wa madini ya dhahabu (“vat
leaching na elusion plants”) kuwa, kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa
Mazingira ya Mwaka 2004, Kifungu cha 81 na Kanuni za Tathmini ya Athari kwa
Mazingira ya Mwaka 2005, zilizofanyiwa marekebisho Mwaka 2018 Miradi yote
inatakiwa kuwa na cheti cha Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM) au Cheti cha
Ukaguzi wa Mazingira (Environmental
Audit).
Kifungu
Na 7 cha Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004 kinasisitiza umuhimu wa kulinda,
kutunza na kusimamia uhifadhi wa mazingira. Aidha, uwekezaji wowote unatakiwa
kukidhi matakwa ya kisheria hususan katika suala zima la Tathmini ya Athari za
Mazingira. Tathmini ya athari za mazingira ni takwa la kisheria na nguzo muhimu
inayosaidia kuhakikisha athari za mazingira kwenye shughuli za maendeleo
zinapatiwa ufumbuzi mapema (Precautionary Principle).
Kutokuwa
na cheti cha Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM) au Ukaguzi wa Mazingira (Environmental Audit) kwa miradi hiyo ni
kosa kisheria na utachukuliwa hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kufungiwa
shughuli zako. Kwa hiyo, Baraza
linawakumbusha wenye miradi yote ya jinsi hiyo kuwa, lazima miradi iliyotajwa
kwenye Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004 ifanyiwe Tathmini ya Athari kwa
Mazingira (TAM) au Ukaguzi wa Mazingira (Environmental Audit) na kupata cheti
cha Mazingira. Kutofanya hivyo ni kutenda kosa kwa mujibu wa kifungu Na. 81 cha
Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya 2004.
Tamko
hili linafuatia athari kadha za kimazingira zilizobainishwa ambazo
zinazosababishwa na uchenjuaji wa madini ambazo zimepelekea vifo vya mifugo na
kuathirika kwa afya za wakazi kwenye maeneo yanayozunguka shughuli hizo. Hivi
karibani matukio ya vifo vya mifugo na kuathirika kwa afya za wakazi kwenye
maeneo hayo vimeongezeka mbali ya uharibifu mkubwa wa vyanzo vya maji,
mmomonyoko wa ardhi na uchafuzi wa hewa za sumu kuwepo karibu na maeneo ya
makazi.
Kama
huna cheti cha Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM) au Ukaguzi wa Mazingira
(Environmental Audit), Baraza linakutaka kusajili mradi wako ndani ya siku
thelethini (30) kwenye ofisi za Baraza Makao Makuu, Mtaa wa Migombani Mikocheni
Dar es Salaam. Au, unaweza kusajili katika Ofisi za Kanda zilizopo Mikoa ya
Arusha, Dodoma, Kigoma, Mbeya, Mtwara na Mwanza ili kupata cheti hicho. Baraza
linawataka kufanya hivyo mara moja na kutakuwapo na ukaguzi wa kina kutathmini
utekelezaji wa agizo hili, kuazia tarehe 15 June, 2020.
Orodha
ya Wataalamu elekezi kwa ajili ya usajili wa miradi hiyo pamoja na tathmini ya
athari za mazingira na kaguzi za mazingira inapatikana katika Tovuti ya Baraza
(www.nemc.or.tz).
Aidha, Orodha hiyo itatolewa kwa mara nyingine kwenye magazeti yatolewayo kila
siku, pamoja na namba zao za simu.
Wataalamu
elekezi kwa shughuli hii ni wale tu waliokidhi matakwa ya sheria baada ya
kuwasilisha taarifa zao kwa ajili ya kuhuisha daftari (register) la orodha ya
wataalamu elekezi waliosajiliwa kufanya Tathmini ya Athari kwa Mazingira na
Tathmini ya Uhakiki wa Athari za Mazingira.
Wataalam
elekezi vilevile mnakumbushwa kuwa Gharama mnazotoza kwa ajili ya kazi za
tathmini za athari kwa mazingira na kaguzi za mazingira ziwiane na uhalisi wa
shughuli husika. Ili kuweza kuwasaidia wawekezaji hao, Bei ya kazi ya tathimini
iwe gharama ziwe na mchanganuo wa gharama halisi ya kuaganya kazi kwa maana ya
mahitaji ya lazima kwa ajili ya tathmini na kaguzi na itofautishwe bayana na
ada ya mtaalam husika (professional fee).
Kwa
maelezo zaidi piga namba: 0737796252 dawati la malalamiko na msaada
Imetolewa na :
Mha. Dkt. Samuel Gwamaka Mafwenga
Mkurugenzi
Mkuu,
Baraza
la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...