KATIBU Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo ameongoza mazishi ya aliyekua Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Profesa Apollinaria Elikana Pereka aliyefariki Mei 3, 2020 mkoani Morogoro.

 Kabla ya kufikwa na umauti kumkuta Aprili 14, 2020 alipata kiharusi ambapo alilazwa katika Hospitali ya Chuo Kikuu Cha Kilimo (SUA), Morogoro.

Marehemu Profesa Pereka amezikwa leo Mei 7 mwaka 2020 katika kijijini cha Mwangika Kahunda, Sengerema - Mwanza.

Dk.Akwilapo alimwakilisha Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Lazaro Ndalichako ambapo alisema kuwa marehemu Prof.Pereka atakumbukwa kwa utendaji mzuri na usimamizi bora wa taasisi za seikali,  nchini na hata nje ya mipaka ya nchi yetu.

Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Prof. Preksedis Marco Ndomba akitoa salamu za Rambirambi katika ibada ya mazishi ya marehemu iliyofanyika katika kanisa la Katoliki la Mtakatifu Yakobo, naye alisema Taasisi imepoteza Kiongozi shupavu na mlezi mahiri.

"Tumepoteza mlezi ambaye ilikuwa ni vigumu kutenganisha nafasi kubwa aliyokuwa nayo na malezi aliyotupa kiasi cha kuzoea kumuita Mama, hivyo   Taasisi imempoteza Mama," alisema Prof. Ndomba.
 Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia akiweka taji la Maua kwenye kaburi la Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Prof. Apollinaria Elikana Pereka.
 Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Prof. Preksedis Marco Ndomba akiweka taji la maua kwenye kaburi la Marehemu Mama yetu Prof. Apollinaria Elikana Pereka
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Lazaro Ndalichako (Mb).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...