Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
NCHINI
Ecuador miili ya waathirika wa virusi vya Corona imeendelea kuzagaa
mitaani huku tahadhari zaidi ikitolewa dhidi kuenea kwa virusi hivyo.
Baadhi
ya wachunguzi wameonekana katika moja ya mitaa wakichunguza maiti ya
mwanaume wa miaka 65 aliyedaiwa kuambukizwa COVID-19 katika mji mkuu wa
nchi hiyo Quito siku ya Jumanne na baadaye wafanyakazi wa wazishi
walifika na kumweka kwenye jeneza na kumsafirisha, Dailymail imeripoti.
Ecuador ina zaidi ya kesi 31,000 zilizothibitishwa za Covid-19 pamoja na vifo zaidi ya1,569.
Katika
ukanda huo Ecuador ni nchi ya tatu kuathirika zaidi baada ya Brazil
yenye vifo 7,921 na kesi 114,715 na Mexico ambayo imerekodi vifo 2,271
na kesi 26,025.
Wataalam wameeleza kuwa gonjwa hilo litazidi kuenea kwa kasi katika ukanda wa Latin Amerika katika siku zijazo.
Nchi
kadhaa, ikiwemo Ecuador, Colombia na Jamhuri ya Dominika, wameongeza
hatua za kuchukua tahadhari zaidi ikiwa ni sehemu ya kupambana na janga
hilo.
Ikumbukwe kuwa
tangu Ecuador itangaze kisa cha kwanza Februari 29, ukanda wa pwani wa
Guyas ulikuwa na maambuki 4,000 sawa na asilimia 70 huku Guayaquil
ambako ndiko kitovu cha maambukizi miili karibu 800 ilikusanywa kutoka
majumbani na mitaani kwa mwezi Februari ambapo mochwari na kampuni za
mazishi zilielemewa na uwingi wa maiti.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...