Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
HADI
sasa Lesotho haijatangaza kisa cha maambukizi ya homa ya mapafu
inayosababishwa na virusi vya Corona (Covid-19) licha ya majirani zao
Afrika kusini kuwa na kesi za Covid-19 zaidi ya elfu saba na vifo zaidi
ya mia moja, pia Lesotho inakua nchi pekee kati nchi 54 barani Afrika
ambayo haijaripoti maambukizi ya virusi hivyo ila nchi hiyo imeendelea
kuchukua hatua kadhaa ikiwa ni pamoja na kufunga, mipaka, vyuo, shule
pamoja na shughuli nyingine zinazoleta mkusanyiko wa watu.
Baadhi
ya wachambuzi wameeleza kuwa nchi hiyo imekua ikiishi kwa tahadhari
kubwa kutokana na maambukizi ya kiwango cha juu ya Virusi vya UKIMWI
(VVU) vilivyoikumba nchi hiyo katika miaka ya themanini na mwaka 1986
kutangazwa kuwa ni janga la taifa ambalo lilipelekea nchi hiyo kuwa ya
pili duniani kwa kiwango kikubwa cha maambukizi wa VVU.
Wataalamu
wameeleza kuwa huenda sababu ya nchi hiyo kutokupata maambukizi ni
kutokana na maeneo mengi ya nchi hiyo yenye milima kutofikika na nusu ya
idadi ya watu wanaishi vijijini hivyo kuweka vizuizi ni rahisi kuliko
nchi zenye idadi kubwa ya watu (ikumbukwe Lesotho ina watu wapatao
milioni mbili,) Afrika kusini ambayo ipo karibu zaidi na Lesotho
imeathirika na Covid-19 na vizuizi vilivyowekwa vinazidi kuwasaidia
majirani hao.
Nchini
Lesotho asilimia 25 au mtu mmoja kati ya wanne anaishi na maambukizi ya
VVU, huku nusu ya vijana 300,000 ambao ni wanawake (miaka 15 -25)
wanaishi na maambukizi hayo na zaidi ya yatima 200,000 ni zao la VVU,
hii ni kwa mujibu wa Shirika la Afya duniani (WHO.)
Kutokana
na maambukizi hayo tahadhari nchini humo zimekuwa zikitolewa kila siku
na hasa ni kwa kuwahimiza wananchi katika matumizi sahihi ya kondomu
pamoja na kupima afya zao huku kundi la vijana likielezwa kuwa hatarini
zaidi katika janga hilo kwani vijana wengi wanaoingia katika mahusiano
hawajui hali za wenza wao.
Kwa
mujibu wa takwimu zilizotolewa mwaka 2018 inaonesha kuwa watu 340,000
wanaishi na VVU Lesotho huku watu 6,100 wakifa kwa virusi hivyo.
Mapema
wiki iliyopita waziri mkuu wa nchi hiyo Thomas Thabane alihutubia taifa
na kueleza kuwa Serikali italegeza vizuizi vilivyowekwa mwezi jana
ikiwa ni pamoja na kuruhusu uendeshaji wa biashara ila kwa muda maalumu,
kufungua kwa shule na vyuo pamoja na ofisi za umma ambazo zitafunguliwa
na kufungwa kwa muda uliopangwa.
Thabane
aliwataka wananchi kuendelea kuvaa barakoa pamoja na kufuata sheria
zinazotolewa na Wizara ya afya pamoja na Shirika la Afya Duniani.
Hata
hivyo alieleza kuwa mipaka ya nchi hiyo itaendelea kufungwa wakati huu
ambao nchi hiyo inapambana katika kuzuia kuenea kwa virusi hivyo.
Ikumbukwe
kuwa licha Thabane Thomas kuongoza mapambano dhidi ya virusi vya Corona
nchini humo Alhamisi ya wiki iliyopita alitangaza kuachia madaraka
mwisho wa mwezi Julai huku ikielezwa kuwa ni maamuzi ya hiari kutokana
na umri wake lakini wachambuzi wa masuala nchini humo wameeleza kuwa
kuachia madaraka hayo kunatokana kesi ya mauaji ya mkewe ambayo
inamkabili yeye na mke wake Maesaiah Thabane aliyemuoa miezi miwili
baada ya kifo cha mke wake wa kwanza Lipolelo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...