Katibu mkuu wa umoja wa wajasiliamali wadogo wadogo mkoa wa Iringa Joseph Mwanakijiji akiongea na waandishi wa habari baada ya kutokea wimbi la vibaka manispaa ya Iringa kwa kuwaibia wajasiliamali.
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama machinga manispaa ya Iringa wameendelea kuathirika na wizi unaofanywa na vibaka kwa kuvunja stoo na kuiba mali za wajasiliamali hao.
Akizungumza na waandishi wa habari katibu mkuu wa machinga mkoa wa Iringa Joseph Mwanakijiji alisema kumekuwepo na wimbi kubwa la vibaka ambao wanavunja ofisi za wajasiliamali wadogo wadogo na kuiba Mali za wajasiliamali.
Alisema kuwa vibaka wameongezeka katika kipindi hiki cha Corona kutokana na kuongezeka kwa matukio mbalimbali ya wizi unaotokea kwa wajasiliamali wadogo wadogo wa manispaa ya iringa.
Mwanakijiji alisema siku za karibu zaidi ya wajasiliamali kumi na tano walivunjiwa stoo zao na kuibiwa mizigo na Mali zote zilizokuwemo ndani na kupelekea hasara kubwa kwa wajasiliamali hao.
"Wajasiliamali wengi mitaji yao bado midogo na wanamikopo katika taasisi za kibenk au kwa watu binafsi hasa wenye maduka makubwa hivyo unapo muibia mjasiliamali huyu unamrudisha nyuma kibishara na kumfanya awe maskini kabia"alisema mwanakijiji
Alisema kuwa uongozi wa machinga mkoa wa Iringa uliunda kamati maalum ya kuwatafuta vibaka hao kwa ushirikiano mkubwa na serikali ya wilaya ya Iringa na kufanikisha kuwakamata baadhi ya vibaka wakiwa na mizigo ya wizi.
"Tulifanya kazi vizuri kushirikiana mkuu wa wilaya Richard kasesela na jeshi la polisi Iringa tukafanikiwa kukamata baadhi ya bidhaa zilizokuwa zimeibiwa kwenye stoo za wajasiliamali wadogo wadogo hapa manispaa" alisema mwanakijiji
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...