Na Abdullatif Yunus wa Michuzi TV.

Chama cha Ushirika cha Wakulima wa Kahawa Wilaya za Karagwe na Kyerwa (KDCU), kimezindua Mizani 15 mipya ya Kielektroniki yenye thamani ya shilingi Milioni 46, na kugawiwa katika Vyama vya Msingi, wakati tukielekea msimu mpya wa zao la kahawa.

Mizani hiyo imezinduliwa na iliyozinduliwa na kukabidhiwa na Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti katika tukio lililofanyika mapema Mei 21, katika Viwanja vya Chama hicho Wilayani Karagwe, huku tukio hilo likihudhuliwa na Viongozi wa Ushirika, viongozi wa Vyama vya Msingi pamoja na wakulima.

Awali akimkaribisha Mkuu wa Mkoa Kagera, Mkuu wa Wilaya Karagwe Godfrey Mheluka amesema Mizani hiyo imekuja wakati muafaka lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa Mkulima wa zao la kahawa, hanyanyaswi, haonewi na haibiwi wakati wa kuuza zao hilo, na kuongeza kuwa Wilaya ya Karagwe imejipanga vizuri kwa msimu unaoanza hivi karibuni, hakuna magendo yoyote yatakayofanyika

Akihutubia Wadau hao wa zao la Kahawa, Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti amesema Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa Mkulima yeyote wa zao la kahawa atakuwa akilipwa ndani ya masaa 24 mara baada ya kupeleka kahawa yake katika chama cha msingi, hivyo hapatakuwa na ucheleweshwaji wa malipo kwa namna yeyote, na kuahidi kutoa taarifa ya kila mwezi kwa Wananchi Mkoani humo kuhusu mwenendo wa msimu wa kahawa namna ilivyokusanywa, ilivyouzwa na kinachoendelea, na hii itamfanya kila mwananchi hususani Mkulima kuwa na taarifa za wazi juu ya Biashara ya zao hilo na huku akiwataka Viongozi wa Vyama vya Msingi kukutana na kuchukua taarifa kwa wakulima kila baada ya Wiki mbili, na zaidi akisisitiza kufanya vizuri msimu huu kuliko msimu uliopita.

Awali Meneja wa Chama Cha Ushirika KDCU katika salaam zake za Utangulizi pamoja na mambo mengine amedai kuwa KDCU mpaka sasa wameotesha miche laki tatu na kufikia mwezi wa Tisa wanatarajia kuwa na Miche laki tano, ambayo itagawiwa kwa wanachama wake na akiongeza kuwa kwa sasa KDCU wameendelea kuhamasisha wakulima wao kujiunga na Bima ya Afya kwani kunipitia Ushirika gharama ya kujiunga ni kidogo.
 Pichani Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti akisaidiana na Viongozi wengine kukabidhi Moja kati ya Mizani kumi na tano kwa Kiongozi wa Chama cha Msingi.
 Pichani Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti akifurahia moja kati ya Miche inayopatikana katika shamba la Mkulima Bwn. Msafiri Gabagambi Wamara mkazi wa Kata ya Ndama wakati alipomtebelea Mkulima huyo Shambani kwake mapema kabla ya tukio la kukabidhi Mizani.
 Pichani Sehemu ya wadau na Viongozi wa Vyama vya Msingi waliohudhulia tukio la kukabidhiwa kwa Mizani ya Kielektroniki kwa Vyama vya Msingi Wilayani Karagwe kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa zao la kahawa.
 Pichani ni Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Marco Elisha Gaguti akizungumza na wakulima na wadau wa zao la kahawa (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Mizani mipya ya Kielektroniki Wilayani Karagwe.
Pichani Ni Mizani mipya ya Kielektroniki ambayo imekabidhiwa kwa Vyama 15 vya Msingi kwa Wilaya za Karagwe na Kyerwa, vyenye thamani ya Shilingi Milioni 46.
 Pichani ni Meneja wa KDCU Ndg. Osca akisoma taarifa fupi ya Chama cha Ushirika KDCU  kwa Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Marco Gaguti, katika tukio la Kukabidhi Mizani mipya 15 ya kielektroniki kwa vyama vya Msingi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...