Na Woinde Shizza ,ARUSHA

Mtafiti wa Dawa za asili aliyejulikana kwa jina la Rose Roberty (changa Muja) ameiomba Serikali kumsaidia kupima dawa aliyogundua na kuifanyia majaribio kuona kama inatibu ugonjwa wa Corona (Covid-19)

Akiongea na waandishi wa habari  leo  nyumbani kwake,Rose alieleza kuwa  ameweza kugundua dawa ambayo inaweza ikatibu ugonjwa huu ambao unaotikisa dunia ,na anaimani kabisa dawa hiyo itaweza kuponya ugonjwa huo.

Alisema dawa hiyo inatokana na mchanganyiko wa miti shamba mbalimbali iliopo hapa nchini,ambayo ameichanganya pamoja na viungo mbalimbali vikiwemo limao ,tangawizi kitunguu swaumu na vinginevyo .

Alibainisha kuwa  virusi vya ugonjwa huu wa Corona vinashambulia Sana Kinga za mwili na iwapo mtu atajitaidi kutumia vitu vya kuboresha na kuongeza Kinga hizi itasaidia kutopata ugonjwa huu.

" Dawa hii Kama nilivyowaambia ni mchanganyiko wa vitu vingi ambavyo ni miti shamba ,na nimechanganya miti ya Aina mbalimbali ,unajua zamani kule kwetu Singida kunamti ambao tulikuwa tukiumwa Sana kifua Cha kubana au mafua tunatumia na mti huu pia unapendwa na wanyama Sana hivyo nimeuchukuwa na nikachangaya na mingine ndio nikaitengeneza hii dawa"alibainisha Rose

Alisema kuwa tayari yeye na familia yake wameshaitumia dawa hii ambapo alisema kuwa awali ,kunamtu mmoja wa familia yake alikuja nyumbani akiwa na dalili zote za ugonjwa wa Corona na ndipo alipokumbuka miti hiyo alichukuwa akaichanganya na alivyompa alipona ,huku akibainisha mbali na hao pia alishawapa baadhi ya watu ambao walikuwa wanabanwa Sana vifua na wanaendelea vyema.

Alisema awali alipeleka dawa hii Katika sehemu husika ikiwemo mamlaka ya chakula na dawa lakini akusaidika kwani Hawakumsikiliza Bali walimpuuzia na ndipo alipoamua kurudi nyumbani na kuamua kuwaita waandishi ili imsaidie kuomba serikali ,iichukue dawa hii na kuifanyia utafiti.

Aidha alimshukuru Rais Wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania John Magufuli kwa kuweza kuwaruhusu Waganga wa tiba za asili nao kushiriki Katika Zoezi zima la kuangalia namna ya kupata dawa za ugonjwa huu wa Corona pamoja na namna anavyokuwa na Imani ya dawa za miti shamba pamoja na kumuamini Mungu.

Aliongea kuwa anaimani kabisa dawa anayoitengeneza  inaweza ikatibu na kukinga watu  kutokupata ugonjwa huu na iwapo serikali itaipima na kuikubali Basi atapenda itambulike kwa jina  la MJOUNJOU.

Alitoa wito kwa  wananchi pamoja dawa zinaendelea kugunduliwa ni vyema waendelea pia kufuata tahathari zinazotolewa na wataalam wa  afya.
Picha ikionesha Mtafiti wa dawa za asili aliyejulikana kwa jina la Rose Roberty (changa Muja) akionesha dawa ya kutibu ugonjwa wa Corona 19 aliyogundua ambayo ameiomba Serikali imsaidie kuichukuwa na kuipima na kufanyia majaribio (picha na Woinde Shizza,Arusha).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...