Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
MUSTAPHA
Mohammed maarufu kama Mairutuwa na kiongozi maarufu wa genge la utekaji
nyara nchini Nigeria ambalo pia linadaiwa kumuuwa mseminari wa Shirika
la Mchungaji Mwema, Michael Nnadi (18) wa Seminari ya Mchungaji Mwema
katika jimbo la Kaduna mnamo Januari 2020; ameeleza sababu ya kumuua
marehemu Nnadi licha ya kukusanya fidia kutoka kwa seminari hiyo.
Ikumbukwe
kuwa mnamo Januari 9, watu wenye silaha walivamia Seminari hiyo na
kuwateka nyara waseminari wanne ambapo walimuua mmoja wao na
kuwaachilia watatu mnamo Januari 31na hiyo ni baada ya kupata fidia
kutoka kwa seminari hiyo, hata hivyo baadaye mwili wa mseminari wanne,
Michael Nnadi ulipatikana kwenye kichaka mnamo tarehe 2 Februari na
kuzikwa tarehe 11 Februari mwaka huu.
Katika
mazungumzo na gazeti la The Sun, Mustapha amesema tangu siku ambayo
Nnadi alitekwa nyara, alikuwa akimuhubiria injili ya Yesu na kumwambia
usoni mwake abadilishe njia zake mbaya au aangamie na kueleza kuwa
marehemu Nnadi hakumruhusu kuwa na amani kila wakati alikua akihubiri
Injili ya Yesu Kristo kwa ujasiri huku akijua kuwa hawako katika imani
moja jambo lililopelekea kumuua Nnadi.
Mustapha
ambaye kwa sasa yuko mahabusu akiwa washiriki wengine wawili wa genge
lake, amesema kuwa waliamua kuvamia Seminari hiyo kwa sababu walijua
seminari itatoa pesa nzuri na hiyo ni kwa mujibu wa habari juu ya
Seminari hiyo waliyopewa na mwanachama wa genge hilo ambaye ni
mfanyabiashara wa Okada (bodaboda) anayeishi karibu sana na Seminari
hiyo.
Amesema ilichukua karibu siku tano kufanya uchunguzi sahihi juu ya Seminari hiyo kabla ya kuanza operesheni hiyo.
Pia
ameeleza jinsi walivyotumia nambari ya simu ya marehemu Nnadi
kuwasiliana na viongozi wa seminari hiyo na kutaka fidia ya Naira 100
milioni ambayo baadaye ilipunguzwa hadi kufikia Naira 10 milioni
iliyolipwa na viongozi wa Seminari hiyo kwa kutolewa kwa waseminari
watatu.
Mustapha amefunguka
zaidi na kueleza namna walivyowalazimisha viongozi wa shule kununua kadi
za rejareja za mtandao simu na kuweka jumla ya Naira 30,000 na kwenda
nazo mahala walipokuwa wamekubaliana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...