Na Mwandishi wetu
KATIKA kuendeleza Mziki wa Dance hapa nchi Mwanamziki, Patrick Kessy ameachia kibao kipya cha "SIRI" ambacho kinafanya vizuri hivi sasa na kuwaburudisha wapenzi wa mziki hapa nchini.
"Patrick Kessy alikuwa mdau mkubwa wa mziki wa dansi na sasa ameamua kishika mic na kuingia studio na kutoa wimbo wa 'Siri'," amesema meneja Menssah.
Katika wimbo huo, Patrick Kessy amewashirikisha waimbaji nguli wa dansi, Grayson Semsekwa aliyewahi kutamba na bendi za Extra Bongo, Twanga Pepeta na TOT, pamoja na Richard Mangustino 'Teacher'.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...