Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia
Ackson akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya Wauguzi
katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma. Kulia kwake ni Mkuu wa
Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge na kushoto kwake ni Mganga
Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dkt. Ernest Ebenzi.

Baadhi ya Wauguzi wa Hospitali
ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma wakimsikiliza Naibu Spika wa Bunge, Dkt.
Tulia Ackson wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya Wauguzi
Duniani.

Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia
Ackson akikagua ukarabati uliofanyika katika Wodi ya Watoto katika
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma wakati wa kilele cha maadhimisho
ya wiki ya Wauguzi. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt.
Bilinith Mahenge na Wakwanza kulia ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo,
Dkt. Ernest Ebenzi.

Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia
Ackson akikata utepe kuzindua Wodi ya Upasuaji ya Wanawake katika
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma ambayo ilikuwa katika marekebisho
wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya Wauguzi. Kulia kwake ni
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge na kushoto kwake ni Mganga
Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dkt. Ernest Ebenzi.

Baadhi ya Wauguzi wa Hospitali
ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma wakila kiapo cha utendaji kazi wakati wa
kilele cha maadhimisho ya wiki ya Wauguzi Duniani.
PICHA NA BUNGE
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...