Na Abdullatif Yunus MichuziTV.
Pikipiki 27 zilizonunuliwa na Rais John Pombe Magufuli kwa ajili ya kuwasaidia Maafisa Tarafa kote Nchini, kutimiza majukumu yao zimeendelea kukabidhiwa kwa Walengwa ambapo kwa Mkoa wa Kagera Pikipiki hizo zimekabidhiwa rasmi na Mkuu wa Mkoa Brigedia Marco E. Gaguti mapema Mei 22, 2020.
Pikipiki hizo zipatazo 27, aina ya SANLG zenye thamani ya Jumla Shilingi 59,913,000/= tayari zimegawiwa katika Wilaya Nane zinazounda Mkoa Kagera, na Idadi yake kama inavyoonesha katika Mabano, Bukoba(5), Missenyi(2), Karagwe(5), Kyerwa(4), Muleba(5), Biharamulo(2), na Ngara(4).
Akikabidhi Vitendea kazi hivyo kwa Maafisa Tarafa, Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti, amewataka kutumia Pikipiki hizo kuwafikia Wananchi wakiwemo wakulima, katika kuongeza thamani ya mazao ya kibiashara ikiwemo zao la Ndizi na Kahawa, sambamba na kuendelea kusimamia suala la Ulinzi na Usalama hasa Wilaya zile zinazopakana na Nchi jirani.
Akitoa shukrani Mara baada ya kukabidhiwa Pikipiki hizo, kwa niaba ya Maafisa Tarafa wengine Bwn. Jovin Rutainurwa Afisa Tarafa Rwamishenye ameshukuru kwa Serikali ya awamu ya Tano chini ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kununua pikipiki hizo huku akisema kukosena kwa chombo cha Usafiri ilikuwa ni moja kati ya changamoto kubwa zilizowakumba Maafisa hao, na kuahidi kwenda kutekeleza vyema majukumu yao ikiwa ni pamoja na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Pichani Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti akikabidhi Funguo kwa Afisa Tarafa Katerelo, kwa niaba ya wengine, ikiwa ni Pikipiki mpya zilizonunuliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa Maafisa Tarafa Nchi Nzima.
Pichani ni Miongoni mwa Pikipiki tatu kati ya Ishirini na Saba, zenye thamani ya Shilingi Milioni 59,913,000 ambazo zimekabidhiwa kwa Maafisa Tarafa Mkoani Kagera, ikiwa ni ahadi ya Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli lengo ni kuwasaidia Maafisa Tarafa kutimiza wajibu wao.
Pichani ni Afisa Tarafa Rwamishenye Bwn. Jovin Rutainurwa akitoa shukrani zake kwa niaba ya Maafisa Tarafa wengine Mara baada ya kukabidhiwa Pikipiki hizo aina ya SANLG.
Pichani ni sehemu ya Wanahabari, Viongozi na Watumishi wakifuatilia Taarifa ya Tukio la kukabidhi Pikipiki kwa Maafisa Tarafa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...