Na Editha Karlo-Michuzi TV,Kigoma.

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa anatarajia kufanya ziara ya siku moja
mkoani Kigoma leo kwa ajili ya kugawa miche ya michikichi kwa makundi
mbalimbali ya wakulima ikiwa ishara ya kuanza rasmi utekelezaji wa
mkakati wa serikali kuelekea kujitegemea kwa mafuta ya kula
yatakayokuwa yakizalishwa kupitia zao la michikichi.

Mkuu wa mkoa Kigoma,Emanuel Maganga akizungumza na waandishi wa habari mjini Kigoma leo alisema kuwa mpango wa ugawaji wa miche hiyo
utafanyika katika gereza la Kwitanga Halmashauri ya wilaya Kigoma na
kambi ya JKT Burombola kikosi cha 821 wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma.

Maganga alisema kuwa jitihada kubwa zilizokuwa zikifanywa na Waziri
mkuu Majaliwa sasa ndiyo zinaanza rasmi utekelezaji kwa miche
iliyozalishwa kupelekwa kwenye mashamba ya wakulima kwa kupandwa na
ndiyo mkakati rasmi wa kutekeleza mpango wa kuongeza uzalishaji wa
mafuta ya mawese nchini unaanza rasmi sasa.

Akizungumzia nafasi ya mkoa katika kusimamia utekelezaji wa mpango huo
Mkuu wa mkoa Kigoma,Emanuel Maganga alisema kuwa wataalam na watendaji wa mkoa huo wakishirikiana na taasisi mbalimbali wamejipanga kufanya uhamasishaji kwa wananchi, kutoa maelekezo na kufanya tathmini juu ya mpango huo na kwamba tayari wananchi wameonyesha ari kubwa ya
kushiriki kwenye utekelezaji huo.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wizara ya kilimo,Gerlad Kusaya alisema
kuwa tayari miche milioni 1.8 ipo tayari kwa ajili ya kupanndwa
mashambani ikiwa ni sehemu ya mpango wa uzalishaji na usambazaji kwa
wakulima miche milioni tano ambayo itapandwa kwenye mashamba ya
wakulima ili kufikia lengo la tanzania kulima zao la michikichi kwa
wingi kwa ajili ya kujitegemea katika uzalishaji wa mafuta ya mawese
na kuondoa hali ya sasa ya kutumia shilingi bilioni 445 kuagiza mafuta
ya mawese nje ya nchi.

kusaya alisema kuwa katika mpango wa muda mrefu wa serikali kupitia
wizara hiyo wanatarajia kuzalisha miche milioni 15 kwa mwaka na
kuisambaza kwenye mashamba ya wakulima na kuwezesha Tanzania kufikia
lengo la kuzalisha tani 570,000 kwa mwaka ambazo zitatimiza ndoto ya
nchi kuacha kuagiza mafuta ya mawese nje na kufanya manunuzi makubwa
ya fedha za kigeni kwa ajili ya kuagiza bidhaa hiyo.

Hii ni ziara ya nne ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kutembelea mkoa
Kigoma kwa ajili ya kutembelea, kukagua, kuhamasisha na kuona hatua
zinazofikiwa katika utekelezaji wa mpango wa serikali wa kuuchagua
mkoa Kigoma kama mkoa kiongozi katika kilimo cha zao la michikichi na
uzalishaji wa mafuta ya mawese.
Katibu Mkuu wizara ya  kilimo Gerlad Kusaya akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujio wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mkoani Kigoma kuzindua mpango wa upandaji wa zao la michikichi kwenye mashamba ya wakulima mkoani humo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...