UTEUZI WA WAKURUGENZI WA MAMLAKA ZA MAJISAFI NA USAFI
WA MAZINGIRA – ARUSHA NA SUMBAWANGA
Waziri wa Maji Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb) amefanya
uteuzi wa Wakurugenzi Watendaji wa Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira za Arusha
na Sumbawanga kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia leo tarehe 15 Mei, 2020.
Taarifa ya Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Prof. Kitila
Mkumbo imewataja walioteuliwa kuwa ni Mhandisi Justine Gordian Rujomba
anayekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jiji
la Arusha (AUWSA), na Mhandisi Gibon Nzowa anayekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Sumbawanga (SUWASA).
Uteuzi huo umefanyika chini ya Sheria Namba 5 ya
Usambazaji Maji Usafi wa Mazingira ya mwaka 2019. Aidha, Wakurugenzi walioteuliwa watakuwa Makatibu wa
Bodi za Wakurugenzi katika mamlaka hizo.
Kitengo cha
Mawasiliano
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...