NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe amehitimisha ziara yake Chuo Kikuu Mzumbe kwa kutembelea na kukagua ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya kampasi ya Dar-es-salaam Tegeta ambacho kimekusudiwa kuanza kutoa Shahada za Awali Kwa mwaka 2020/2021.

Aidha, amepongeza hatua kubwa iliyofikiwa hadi sasa katika ujenzi wa nyumba za madarasa na mihadhara na   kupendekeza ujenzi unaoendelea kuendana na mahitaji ya sasa ya mabadiliko ya teknolojia, kwa kuwezesha matumizi ya teknolojia katika ufundishaji.

Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Naibu Makamu Mkuu chuo Prof Ernest Kihanga amesema ukarabati huo ulianza Juni 2018 ukiwa ni upanuzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam na kwamba ujenzi umekamilika kwa asilimia 99, na majengo yako tayari kuanza  kutumika pindi idhini ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) itakapotolewa.

Amesema chuo hicho kitakuwa na Maktaba, ofisi za walimu, vyumba vya madarasa na mihadhara, chumba cha komputa na huduma nyinginezo muhimu kumwezesha mwanafunzi kusoma. 

Kuanzishwa kwa programu za Shahada za awali kwa Kampasi ya Dar-es-Salaam kutaongeza wigo wa vijana wengi zaidi kujiunga na elimu ya juu nchini sambamba  na kuongeza fursa za ajira. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasiri katika chuo kikuu cha Mzumbe kampasi ya Dar es Salaam-Tegeta, kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya ukarabati na ujenzi wa Vyumba vya madarasa.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhPtex4nRrV_fiGyghVHn6R0udCsjGmccoiq5e-Yys5AlGtS6TkBvMBa-z72Nk5keHJekP42xD-fTGxA6rut-wXVLJXK92syKkfxFbBmJsLbMVMiom4KzsuNKgBDdDAzP3RM0xg/s640/WhatsApp+Image+2020-05-15+at+4.29.32+PM.jpeg
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe akiwa ameambatana na wafanyakazi wa chuo kikuu cha mzumbe wakitembelea majengo ya  chuo kikuu cha Mzumbe jijini Dar es Salaam leo.
C:\Users\HP\Desktop\TEGEZA ZA KUTUMA\WhatsApp Image 2020-05-18 at 16.01.52 (1).jpeg
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe akikagua  moja ya madarasa ya Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam- Tegeta ambako Shahada za Awali yanaterajiwa kuanza. 
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgEi2YsOGkBQMe6MrE8amL1rF3hcNr7Mzb8LLDlzsoK5LTO18BJx_yYeuAKJqZrsy2yC-7SvM1AhH1bACYML7ONPnhMazcZKEDtnCxjf7cl5eAYaiEw5BlBwLKhhrU2sm10hbaP/s640/WhatsApp+Image+2020-05-15+at+4.31.33+PM.jpeg
 Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe (Utawala na Fedha), Profesa Ernest Kihanga akitoa maelekezo kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi na ukarabati wa majengo ya Kikuu cha Mzumbe- Tegeta jijini Dar es Salaam.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhA8e263dhqBCRKrpX3kaxlgH0PcFdeZYmmb9MF4XpxB7S409JXNKyfAbutIh5xf-GjQSiv_teh_lGFkyuHjlje5Okn2K4DS_FFbq3IG0MtsNV2SdIv0FWmF6j1HzBiD8zbBbmj/s640/WhatsApp+Image+2020-05-15+at+4.31.58+PM.jpeg
Mkuu wa Kampasi ya Dar es Salaam, Honest Ngowi akionesha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe baadhi ya maeneo yanayoendelea kukarabatiwa (hayapo pichani) wakati wa ziara yake katika majengo ya Chuo Kikuu Mzumbe tegeta Dar Es Salaam. 
C:\Users\HP\Desktop\SELECTED\IMG_8341.JPG
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe akikagua  miundombinu na madarasa katika Chuo Kikuu cha Mzumbe  Dar es Salaam-Tegeta. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...