NA BALTAZAR MASHAKA, Mwanza
WAUMINI wa madhehebu ya Khoja Shia Ithna Asheria, jijini Mwanza wamejitosa kwenye mapambano ya vita dhidi ya Homa kali ya Mapafu inayosababishwa na Kirusi cha Corona (Covid-19) kwa kutoa msaada wa vifaa kinga vya ugonjwa huo kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza.
Vifaa kinga hivyo barakoa 300, vitakasa mikono 500 na chupa 500 za sanitizer vilikabidhiwa juzi kwa Ofisa Mnadhimu wa jeshi hilo mkoani humu, Safia Jongo kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Jumanne Muliro.
Akikabidhi vifaa hivyo Mwenyekiti wa Bilal Muslim Mission Of Tanzania tawi la Mwanza na Kanda ya Ziwa Alhaji Sibtain Meghjee kwa niaba ya uongozi wa kina mama na vijana wa msikiti huo wa Shia Ithna Asheria, alisema umetolewa ili kuunga mkono juhudi za serikali na kutambua mchango wa jeshi la polisi katika kuhakikisha wananhudumia wananchi wakiwa salama.
“Askari polisi ni wadau muhimu kwa sababu wanahudumia wananchi wengi hivyo kwa kutambua hilo tumeona vema msaada huu tuuelekeze kwao ili wanapowahudumia wananchi wawe na vifaa kinga kwa ajili ya usalama wa afya zao na jamii wanayoihudumia,”alisema Meghjee abaye pia ni Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation, tawi la Tanzania.
Akipokea msaada huo, Jongo aliwashukuru waumini wa madhehebu ya Shia kwa msaada huo na kuomba wasisite kuwasaidia tena endapo fursa kama hiyo itapatikana ikizingatiwa ugonjwa wa corona ni janga la kidunia na akatoa rai kwa askari kuhakikisha wanautumia msaada huo vizuri kwa ajili ya kujilinda na kuchukua thadhari muda wote.
Waumini hao wa Shia Ithna Asheria wamekuwa wa kwanza jijini Mwanza kujitoa kutoa msaada wa vifaa kinga kwa ajili ya askari polisi kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa corona.
Mwenyekiti wa Bilal Muslim Mission of Tanzania, tawi la Mwanza na Kanda
ya Ziwa, Alhaji Sibtain Meghjee kwa niaba ya waumini wa Khoja Shia
Ithna Asheria jijini humu akimkabidhi Ofisa Mnadhimu wa Polisi, Safia
Jongo (kulia) kwa niaba ya Kamanfa wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne
Muliro, msaada wa barakoa 300, sanitizer chupa 500 na vitakasa mikono
500 kwa ajili ya askari wa jeshi hilo kujikinga na virusi vya corona.
Mwenyekiti wa Bilal Muslim Mission of Tanzania, tawi la Mwanza na Kanda
ya Ziwa, Alhaji Sibtain Meghjee (katikati) akiwa na baadhi ya maofisa wa polisi Mkoa wa Mwanza baada ya
kukabidhi barakoa, vitakasa mikono na sanitizer kwa jeshi hilo juzi
katika mapambano ya kujikinga na corona, msaada huo ulitolewa na waumini
wa dhehebu la Khoja Shia Ithna Asheria la jijini humu.Picha zote na
Baltazar Mashaka
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...