Na Khadija Seif, Michuzi tv

MSANII wa Bongofleva Zuwena Mohammed a.k.a Shilole (pichani) amejipanga kutengeneza baba Bora 2020 na kupunguza vifo vya wakina mama kupitia jukwaa la "Tunaweza.

Akizungumza na waandishi wahabari jijini Dar es salaam wakati akitangazwa rasmi kuwa balozi wa jukwaa la "Tunaweza" kupitia taasisi ya Smart Generation inayolenga kutoa elimu pamoja na kubadili mitazamo mibaya kwa vijana pamoja na jamii kwa ujumla Shilole amesema akiwa kama mama yupo tayari kupunguza idadi kubwa ya vifo vitokanavyo na uzazi hasa kwa wakina mama wakati wa kujifungua.

"Nina watoto wawili, najua changamoto kwa wakina mama wakati wa kujifungua hivyo vifo vinaweza kuepukika endapo mama atafata taratibu kutoka kwa mtoa huduma yaani muuguzi ,"amesema shilole

Shilole pia amekemea dhana iliyojengeka katika jamii juu ya baba kijacho kumsindikiza mama kijacho hospitali ni ushamba au kujishusha thamani hivyo kwa kutumia kampeni hiyo ya "Tunaweza" atahakikisha wanaume wote wanaweza na wanahakikisha wanafika hospitali wakiwa na wenza wao .

"Kumpeleka mke au mtarajiwa wako kituo cha afya si ushamba bali ni kuonyesha thamani na hali ya kumjali mwenza wako pamoja na mtoto mnaetarajia kumpata huku kufata maelekezo yanayotolewa kituoni hapo na kuchukua tahadhari Kama kumkinga dhidi ya magonjwa hasa maralia,"

Pia ameeleza namna jinsi watu wote watakavokua wanapata elimu jinsi ya kuwa baba bora,mama Bora na kuwakinga wamama wajawazito na magonjwa hasa maralia,kifaa cha mimba,virusi vya ukimwi na mengine.

"Kutokana na ugonjwa wa virusi vya corona (covid 19) ulivoingia na unavoendelea kuwachukua wapendwa wetu hatuna budi kutoa elimu kupitia radio , mitandao ya kijamii pamoja na filamu fupi fupi kupitia Tv ili kuepuka misongamano ,"

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...