Mwenyekiti wa Taasisi ya Amani Tanzania Sadiki
Godigodi(kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo Mei 20 jijini Dar
es Salaam wakati akielezea taasisi hiyo inavyomuunga mkono Rais Dk.John
Magufuli katika mapambano dhidi ya janga la Corona.Katikati ni Mkurugenzi wa
Siasa na Dini wa taasisi hiyo Alhaji Dk.Sule Seif na kushoto ni Mshauri wa taasisi
hiyo Issa Mkalinga.
Mshauri wa Taasisi ya Amani Tanzania Issa
Mkalinga (kushoto) akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo.Wengine ni Mkurugenzi
wa Siasa na Dini wa taasisi hiyo Alhaji Dk.Sule Seif(katikati) na Mwenyekiti wa
taasisi hiyo Sadiki Godigodi.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Amani Tanzania Sadiki
Godigodi(kulia) akisisitiza jambo kwa waaandishi wa habari wakati wa mkutano
kati ya taasisi hiyo na waandishi wa habari.Wengine ni Mshauri wa taasisi hiyo Issa
Mkalinga(kushoto) na Mkurugenzi wa Siasa na Dini wa taasisi Alhaji Dk.Sule Seif.
Na Said Mwishehe, Michuzi TV.
TAASISI ya Amani Tanzania imewaonya baadhi ya
wanasiasa nchini ambao wanatumia nguvu katika janga la Corona kufanikiza adhima
zao za kisiasa, ni vema wakati huu wakatumia nguvu hiyo hiyo kuunga mkono
juhudi za Rais Dk.John Magufuli na timu yake ili kupambana ugonjwa huo ambao
umekuwa vita kubwa.
Imesema ni vema wanasiasa wa aina hiyo wakaacha
kupotosha na kuwatia hofu wananchi kwa kueleza kuwa Tanzania haijafuata ushauri
na maelekezo ya Shirika la Afya Duniani(WHO) na badala yake wajenge umoja ,
ushirikiano na kuilinda nchi yao kwa kutoa mawazo mazuri yatakayoleta faida kwa
wananchi wote sasa na vizazi vijavyo .
Hayo yameelezwa leo Mei 20 jijini Dar es Salaam
wakati viongozi wa ngazi za juu wa Taasisi ya Amani Tanzania walipokutana na
waandishi wa vyombo vya habari nchini kwa lengo la kuelezea namna ambavyo
wamefurahishwa na hatua ambazo zimechukuliwa na Rais Magufuli kukabiliana na
Covid-19.
Mkurugenzi wa Siasa na Dini wa Taasisi hiyo ya
Amani Tanzania Alhaji Dk.Sule Seif amesema kuwa jambo kubwa la kumpongeza Rais
Magufuli katika kulishugghulia janga la Corona ameweka msimamo thabiti juu ya
kumuamini Mwenyezi Mungu na kutofunga nyumba za ibada na kuendesha dua na
maombi mbalimbali ili kukabiliana nalo janga hilo kwa msaada wa Mungu.
Dk.Sule amesema hatua hiyo imeleta tija kubwa
kwani makadirio ya vifo pamoja na maambukizi yaliyokuwa yamekadiriwa na WHO
hayakufikia yalivyotarajiwa."Jambo ambalo tunaamini maombi yetu Watanzania
yamejibiwa na Mwenyezi Mungu.Hivyo hatuoni sababu ya Corona kutumiwa na baadhi
ya wanasiasa kama mtaji wa kufanikisha mambo yao, bali tuungane na Rais kwenye vita
hii."
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Sadiki Godigodi amesema kuwa taasisi
yao imekuwa ikiwaita waandishi wa habari mara kwa mara hasa linapotokea jambo
linalohusu Taifa na maslahi mapana kwa nchi.Hivyo wameona haja ya kuzungumzia
hotuba ya Rais Dk.Magufuli aliyoitoa Mei 17 mwaka huu akiwa kwenye Ibada
iliyofanyika Kanisa la KKKT Usharika wa Chato mkoani Geita.
Godigodi amesema Rais kwenye hotuba hiyo
amezungumzia mambo mengi ya msingi na yenye maslahi kwa Taifa kutokana na
sababu hizo wameona haja ya kuungana naye katika hotuba yake hiyo ili
kumpongeza na kuendelea kumtia moyo.
"Kwanza kabisa kuendelea kumpongeza kwa
msimamo usiyoyumba kuhusu vita dhidi ya ugonjwa wa Covid-19 , miongoni mwa hayo
ni kutoiweka nchini kwenye Lockdown , jambo ambalo lingeleta maafa makubwa kwa
jamii yetu kuliko ugonjwa wenyewe.Pia hata nchi ambazo zimeweka sheria hiyo
imeonekana ni kuwatesa wananchi wake , jambo ambalo limeleta vurugu katika
baadhi ya nchi.
"Na katika nchi nyingine wameamua kuindoa
sheria hiyo ili wananchi waendelee kujitafutia riziki zao jambo ambalo kwa hapa Tanzania Rais wetu aliliona mapema
na hakuwa tayari kuwatesa wananchi wake , hii inathibisha kwamba Rais Magufuli
ni kiongozi anayezingatia maisha ya wanyonge,"amesema Godigodi.
Ameongeza kuwa taasisi hiyo imeendelea
kushuhudia namna ambavyo mataifa mengine duniani yanavyofuata mbinu anazotumia
Rais Magufuli katika vita dhidi ya Corona."Mtakumbuka mambo kadhaa aliyoyasema
Rais na sasa ndio yanatokea, mfano Rais wetu alieleza kuwa virusi vya Corona
havifi kwa kunyunyuzia dawa ya kuua wa wadudu , tumesikia WHO likiunga mkono
kauli hiyo ya Rais."
Pia Rais Magufuli alisema kuwa mazingira ya
ugonjwa wa Covid-19 yataendelea kuwepo kama ilivyo kwa magonjwa mengine na
hivyo kuwataka watanzania wasijenge hofu na badala yake wachape kazi huku
wakiendelea kuchukua tahadhari muhimu dhidi ya kujikinga na ugonjwa huo
zinazoendelea kutolewa na watalaam wa afya nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...