Taasisi ya pamoja iliyopo Mbweni inayojishughulisha
na masuala ya Ufundi wa Vyombo vya Moto na Ushoni Zanzibar kwa kushirikiana na
Chama cha Msalaba Mwekundu Kanda ya Unguja vimetoa msaada wa Vifaa mbali mbali
vya kupambana na Virusi vya Corona hapa Nchini.
Vifaa hivyo ni pamoja na Mifereji Hamsini
iliyotengenezwa Kitaalamu kulingana na mazingira halisi ya kujiepusha na Virusi
vya Corona, ndoo 65, Sabuni pamoja na Vitakasa Mikono.
Akikabidhi Vifaa hivyo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Shaaban Seif Mohamed, Mwakilishi wa
Taasisi ya Pamoja Bwana Christhart Scholz alisema Taasisi yake imekuwa ikitoa
taaluma kwa Vijana katika masuala ya Ufundi wa Gari pamoja na Ushoni.
Bwana Chriss alisema Wataalamu wake kwa vile
wamebobea katika masuala ya Ufundi walilazimika na kuamua kutengeneza Mifereji
iliyo salama bila ya kuguswa kwa mikono na mtumiaji mara tuu baada ya kuibuka
kwa janga la kuendea kwa Virusi vya Corona hapa Nchini.
Naye kwa upande wake Mratibu wa Chama cha Msalaba
Mwekundu {Red Cross} Zoni ya Unguja Nd. Soud Kudra Mponzemenya alisema Taasisi
yake kwa kushirikiana na ile ya pamoja tayari wameshajipanga kusambaza Maski hizo
Elfu 10,000 katika maeneo mbali mbali hapa
Nchini.
Nd. Soud alifafanua kwamba usambazaji huo utakwenda
sambamba na Watendaji wa Taasisi hizo kutoa elimu kwa Wananchi hasa Vijijini
juu ya namna Jamii itakavyoweza kuendelea kujiepusha na maambukizi ya Virusi
thakili vya COVIC – 19 ambavyo kwa sasa vimeleta mtafaruk Dunia nzima.
Akitoa shukrani kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd.
Shaaban Seif Mohamed alisema msaada huo wa vifaa unaoleta faraja kwa Serikali
Kuu na Jamii kwa ujumla utasambazwa maeneo mbali mbali Nchini kadri mahitaji
yatakavyoruhusu.
Nd. Shaaban aliwakumbusha Watendaji wa Taasisi
zinazojitolea kusaidia zana na Vifaa vya mapambano dhidi ya Virusi vya Corona
ni vyema wakazingatia ushauri wa Wataalamu wa Afya ili kile wanacho kitengeneza
kiwe katika ubora unaohitajika Kitaalamu. 

Mwakilishi wa Taasisi ya Pamoja
inayojishughulisha na utoaji wa mafunzo ya Ufundi wa Gari na Ushoni Mbweni
Bwana Christhart Scholz akimkabidhi Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Nd. Shaaban Seif Maski 10,000 kwa ajili ya kusambazwa kwa Wananchi
mbali mbali Nchini.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Shaaban Seif Kulia akipokea Ndoo 65 pamoja na
Mifereji 65 iliyotolewa na Taasisi ya Pamoja kwa kushirikiana na Red Cross Zoni
ya Unguja.
Nd. Shaaban Seif Mohamed
akiyashukuru Makampuni, Taasisi na Jumuiya za Kiraia zinazoendelea kuiunga
mkono Serikali Kuu katika mapambano yake dhidi ya kuzuia kuenea kwa Virusi vya
Corona Nchini.
Mwakilishi wa Taasisi ya Pamoja
inayojishughulisha na utoaji wa mafunzo ya Ufundi wa Gari na Ushoni Mbweni
Bwana Christhart Scholz akielezea Taasisi yake ilivyoamua kujitolea katika
mapambano dhidi ya Corona.
Mwakilishi wa Taasisi ya Pamoja
inayojishughulisha na utoaji wa mafunzo ya Ufundi wa Gari na Ushoni Mbweni
Bwana Christhart Scholz akielezea Taasisi yake ilivyoamua kujitolea katika
mapambano dhidi ya Corona.
Baadhi ya Vifaa vya mapambano
dhidi ya Corona ambavyo ni Mifereji, Ndoo na vitakasa Mikono ambavyo Mtu
anaweza kutumia bila ya kugusa kwa mkono.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...