Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii asubuhi hii inaeleza kuwa, Mwanamuziki mkongwe wa Bendi ya Kilimanjaro maarufu kama wana njenje, Mabrouk Hamis Omar almaarufu kama Babu Njenje amefariki dunia leo jijini Dar es salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Akizungumza nasi kwa njia ya simu, Mmoja wanamuziki wa bendi hiyo, John Kitime amesema "Ni kweli Babu Njenje amefariki na sasa naelekea pale alipokuwa akiishi, Mtaa wa Mindu Upanga ambapo taratibu zitafanyika".
Babu Njenje atakumbukwa kwa nyimbo zake nyingi zikiwemo Njenje, Kinyaunyau na nyingine nyingi.
Taarifa zaidi tutawaletea hapo baadae.
Inna lillah wainna ilaih rajiun.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...