Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
RAIS
wa Marekani Donald Trump ameendelea kulituhumu Shirika la afya Duniani
(WHO) kwa kushindwa kuwa chombo huru katika kupambana na janga la
mlipuko wa homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona
(Covid-19.) Ambavyo hadi sasa vimesambaa duniani kote na hakuna chanjo
wala kinga iliyopatikana hadi sasa.
Kupitia
barua aliyoiweka katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram
akiielekeza kwa Mkurugenzi wa WHO Dkt. Tedros Adhonom Ghebreyesus Trump
amesema, aliamua kusitisha michango ya nchi yake kwa Shirika la Afya
Duniani( WHO) tangu Aprili 14 mwaka huu ili kufanya uchunguzi juu ya
mambo ambayo anadai WHO ilizembea kuyafanya katika kupambana na mlipuko
wa virusi vya Corona (Covid 19.)
Pamoja na mambo mengine mengi Trump anasema uchunguzi umebaini yafuatayo;
WHO haijatoa taarifa kwa wakati hasa kwa kutangaza kuwa virusi vya Covid-19 kuwa janga la ulimwengu.
Pia
ameeleza kuwa WHO imetoa taarifa za uongo na za kuaminisha dunia kwamba
Covid -19 haiambukizwi kwa mtu na mtu licha ya baadhi ya wataalamu
kueleza namna ya virusi hivyo vinavyosambaa.
Vilevile
amesema kuwa WHO haikufanya utafiti wake kwa uhuru kupitia wataalamu
wake na badala yake wakategemea taarifa za China na kuihabarisha dunia
jambo ambalo huenda ilikuwa upotoshaji.
Aidha
amelituhumu shirika hilo kwa kuendelea kuisifu China kwamba wanafanya
kazi nzuri hata baada ya wao kuzuiwa kufika Wuhan kwenye kitovu cha
ugonjwa mapema badala yake kuruhusiwa mwishoni kabisa ambapo ugonjwa
ukiwa umeshaenea dunia nzima.
Waraka
huo umeeleza kuwa WHO haikuwaonya China juu ya ubaguzi na unyanyasaji
wa watu weusi wanaoishi China kwa madai kwamba ndio waliosababisha
kuenea kwa Virusi vya Corona na hiyo ni baada ya mabalozi wa nchi za
Afrika kuandika barua kwa Serikali ya China kuhusiana na ubaguzi wa
wananchi wa mataifa ya Afrika.
Kupitia
waraka huo pia imeelezwa kuwa WHO iliikosoa USA kwa kuzuia wachina
kuingia Marekani wakati huohuo ikiisifu China kwamba inalinda Dunia.
Zaidi
sana Trump amemlaumu mkurugenzi wa WHO kwa kutoonyesha uwezo kama
mtangulizi wake ambaye mwaka 2003 aliongoza Dunia kupambana na mlipuko
wa homa ya Severe Acute Respiratory Syndrome (SARS) ambapo aliionya
China kuacha kutoa taarifa za kupotosha ambazo zitahatarisha usalama wa
ulimwengu.
Hivyo Trump
ametoa siku 30 kwa WHO kujirekebisha vinginevyo ataondoa kabisa bajeti
yake ya kuchangia WHO na atafikiria kama kuna umuhimu wa kuendelea kuwa
mwanachama tena kwa sababu hawezi kutumia pesa za walipa kodi wake
kwenye mradi ambao hauna maslahi.
RAIS
wa Marekani Donald Trump
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...