Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
MWANDIKO
wa mwanafunzi Prakiti Malla (16) maarufu kama "Microsoft Word" binti
kutoka Nepal umevunja rekodi ya kuwa mwandiko bora zaidi kuwahi kutokea,
katika mitandao mbalimbali ya kijamii hati za mwandiko wa binti huyo
zimekuwa zikisambaa na kusifiwa kwa namna ulivyoumbwa kwa namna kuvutia
na kusomeka kwa urahisi.
Baadhi
ya watu wamekuwa wakitumia muda mwingi zaidi katika shule za awali
katika kuumba herufi na stadi za uandishi na wachache hufanikiwa kuumba
herufi kwa usahihi huku wengine wakipata wakati mgumu kwa kushindwa
kuumba herufi na kuwa na miandiko mibovu.
Baadhi
ya wataalamu hasa walimu wanaeleza; kuwa na stadi nzuri ya kuandika
haina faida kwa msomaji pekee bali huvutia kwa namna ambavyo
umepangiliwa.
Prakiti
akiwa darasa la nane mwaka 2017 hati za mwandiko wake zilisambaa na
kuzua mijadala katika mitandao ya kijamii hasa Twitter, mwandiko huo
ulionekana kuwa bora zaidi kuwahi kutokea kwa mwanafunzi, herufi
zilikuwa zimeundwa vyema na wengi wamekuwa wakifananisha mwandiko wa
Prakiti na maandishi katika kompyuta.
Mwandiko
wa Prakiti ulipelekea Serikali ya Nepal kuanzisha mashindano ya
"Penmanship Competition" ambapo binti huyo aliibuka kidedea na serikali
ikatangaza mwandiko wa Prakiti ni bora zaidi nchini humo.
Vyombo mbalimbali vya habari vilimnukuu Prakiti akieleza kuwa anatumia masaa mawili kwa siku kwa kufanya mazoezi ya kuandika.
Ni mwandiko pekee uliowafanya watumiaji wa mitandao kufikiria kuuweka mwandiko wa Prakiti katika hati za kompyuta.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...